Novemba , 29 , 2024 : Sia Martin Mlay Mwanafunzi wa Chuo Cha Ardhi – Jijini Dar Es Salaam ( katikati ) ni mmoja wa Washindi wa MILIONI TANO , Kampeni ya Magifti ya Kugifti inayoendeshwa na Kampuni ya Mawasiliano ya Yas ( Zamani Tigo ) ikiwa ni Wiki ya Tatu , Sia ameshinda zawadi hiyo ya Shilingi Milioni tano kwasababu amekuwa akifanya Miamala mbalimbali kama vile kununua Vifurushi , Kulipa Bili , LUKU , Kulipia ada n.k kupitia Mixx by Yas ( zamani Tigo Pesa ) , Bado una nafasi ya kushinda fanya miamala na Mixx by Yas uibuke mshindi kwa maana bado takribani wiki 10 za kutoa zawadi za Simu na Pesa Taslimu kuanzia Milioni 1 – 5. ( Katika Picha Kushoto ni Haji Manara Msemaji wa Kampeni ya Magfiti ya Kugifti , na Kulia ni Bi. Angelica Pesha Afisa Mkuu wa Mixx by Yas.
Na Mwandishi wetu.
Kampuni ya Mawasiliano ya YAS ( zamani Tigo ) , imekabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi 7 wa Kampeni ya “Magift ya kugift” kwa wiki ya 3 ambapo kati ya hao 6 wamejishindia kiasi cha Shilingi Milioni 1 kila mmoja
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo kwa washindi Afisa mkuu wa Mixx by Yas Bi. Angelica Pesha amesema anayofuraha kuona wanakabidhi zawadi kwa washindi kwa wiki ya tatu 3 nakudai kuwa hii ni sehemu ya utaratibu wao kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu na zawadi nyinginezo katika kipindi hiki cha kuelekea siku kuu za mwisho wa mwaka.
Pesha amesema mpaka sasa wameshatoa zawadi za fedha zenye thamani ya kiasi cha TSh milion 35 kwa washindi wa makundi tofauti ikiwemo,mawakala,na wateja wengine.
Kwa upande wake Sia Martin Mlay ambaye amejinyakulia kiasi cha Shilingi mili 5i “ameishukuru Yas kwa kuleta kampeni hiyo ya “MAGIFT ya KUGIFT 2024” na hatimaye yeye kuibuka mshindi, na amewaomba watanzania kushiriki kampeni zinazoletwa na Yas Tanzania kwani hakuna ubabaisha kila mtu anashinda kutokana na bahati yake amesema Mlay.
Nao baadhi ya washindi wengine ambao wamejishindia zawadi ya TSh Milion 1 wameshukuru kwa kupata zawadi zao, ambapo wengi wao Wamesema, pesa hizo wanakwenda kuziendeleza huku wengine wakiahidi kwenda kulipia ada za shule na huduma nyingine muhimu.
Kampuni ya YAS imekuwa na muendelezo mzuri WA kuendesha kampeni mbalimbali ikiwa sehemu ya kujitangaza itakumbukwa kuwa kampuni ya YAS ilizinduliwa hivi karibuni ikichuka pahala la Tigi ambayo imedumu kwa kipindi cha miaka 30 ikitoa huduma zake hapa nchini, na kutunukiwa Tuzo mbali mbali ndani na Nje ya nchi.
Kwa upande wake Msemaji wa Kampeni ya Magifti ya Kugifti Haji Sunday manara amewataka wateja WA Yas kuendelea kutuma miamala kupitia simu zao ili wawe kwenye nafasi nzuri za kujishindia zawadi nyingi, na amesema Wazi kuwa hakuna longol ongo kwenye kampeni hii ya MAGIFT ya KUGIFT, hivyo kila mtu anaweza kuibuka mshindi siku yake ikifika.