Home Kitaifa MWAMBAO, NORAD WAUNGA MKONO JITIHADA ZA KUZUIA UVUVI HARAMU MKINGA

MWAMBAO, NORAD WAUNGA MKONO JITIHADA ZA KUZUIA UVUVI HARAMU MKINGA

Na Boniface Gideon -MKINGA

Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania, chini ya ufadhili wa NORAD wamekabidhi Boti ya kisasa kwa ajili ya kufanya doria kulinda rasilimali za bahari na pwani katika Muktadha wa kudhibit uvuvi haramu. Boti hiyo ni ya pili kutolewa wilayani Mkinga kwa jumuiya za kamati ya uhifadhi wa Bahari ya eneo moja la uvuvi (CFMA- collaborative Fisheries management area) ya Boma Mahandakini yeye vijiji tisa. Kutolewa kwa boti hii litasaidia kuongeza wigo wa doria za ulinzi kwa Vijiji zaidi ya 9 vya kata za Boma na Moa.

Akikabidhi Boti hiyo leo pamoja na Vifaa vyake kamili yenye thamani ya takribani Tsh. miliioni 40 kwa ajili ya doria pamoja na vifaa vyake kamili kama mashine, vifaa vya mawasiliano zikiwemo Simu za mkononi na vinasa sauti za redio, vifaa vya kujiokoa, vifaa vya huduma ya mwanzo pamoja na darubini. Mradi huo utawanufaisha Wakazi wa kata za Boma na Moa wilayani humo.

Mratbu wa Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania Mkoa wa Tanga, Ahmad Salim Omar amesema lengo la kutoa Boti hiyo ni kuwasaidia wavuvi kamati kwa ajili ya kuendesha doria zenye tija Baharini ili kudhibiti uvuvi haramu na hii inakwenda sambamba na kauli mbiu ya Mwambao ya Afya ya Bahari ni Utajiri wa jamii_ ‘ocean health is Community wealth’

“Boti hii ni ya kisasa tunaikabidhi rasmi kwenu Wanaboma mahandakini ikiwa na Vifaa vyake kamili kwa ajili ya doria. Botii hii baada yaa kufika tulitaka ianze, hatukutaka kulala na kwa kipindi cha miezi miwili imeweza kukamata vyombo mbalimbali vya baruti na milipuko, wavuvi haramu na wale wasio na leseni za uvuvi. Kuna wavuvi haramu ambao wameshakamatwa na wamelipa faini takribani mil.5, hii kwa maana nyingine imeisaadia Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kuongeza mapato yake ambayo ni muhimu katika shughulii za uhifadhi na usimamizi wa rasilimali za bahari” Aliongeza Ahmad Omar

Aidha aliwataka Wakazi wanaoishi Mwambao wa Bahari Kutunza rasilimali Bahari ili kuongeza uzalishaji wa Samaki na kipato.

“Lengo letu kama Shirika ni kuwasaidia wavuvi kuongeza kipato chao, endapo kutafanyika uvuvi salama kiwango cha uzalishaji wa Samaki kitaongezeka, nawaomba mtunze rasilimali za Bahari lakini pia naomba matumizi sahihi ya boti hii na utunzaji ili kifanye kazi iliyokusudiwa na Shirika” amesisitiza Omar

kwa upande wake Katibu tawala Wilaya ya Mkinga Parango Abdul amelishukuru shirika hilo kwa msaada huo wa kusaidia juhudi za kutunza rasilimali za Bahari.

“Tunawashukuru sana Mwambao Coastal Community Network Tanzania pamoja na Wadau wa NORAD kwa juhudi zenu za kusaidia mapambano dhidi uvuvi haramu, lakini pia mnaisaidia serikali, niwaombe Wananchi wenzangu msiwaangushe Wadau hawa, tunataka tuone juhudi zao zinaleta matokeo chanya kwa Jamii yetu, tunzeni rasilimali Bahari ili muongeze kipato chenu” ameongeza Parango

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!