Home Kitaifa MWALIMU WA SHULE YA MSINGI KAKANJA WILAYA KYERWA ALIYE WACHAPA VIBOKO KIKATILI...

MWALIMU WA SHULE YA MSINGI KAKANJA WILAYA KYERWA ALIYE WACHAPA VIBOKO KIKATILI WANAFUNZI ASIMAMISHWA KAZI MARA MOJA.

Na Theophilida Felician Kagera.

Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Kakanja iliyopo kata ya Kakanja wilaya Kyerwa Mkoani Kagera amesimamishwa kazi akituhumiwa kuhusika na tukio la kuwachapa viboko kikatili wanafunzi wawili wa darasa la nne shuleni hapo.

Akizungumzia juu ya tukio hilo kwa waandishi wa habari ofisini kwake Manispaa ya Bukoba Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe Albert Chalamila amesema kuwa hatua hizo zimechukuliwa nauongozi wa Mkoa kufuatia kusambaa katika mitandao ya kijamii video ikimuonyesha mwalimu Mkuu wa shule hiyo ya Kakanja Isaya Benjamini Emmanueli akitekeleza tukio la kuwaadhibu kwakuwachapa viboko kikatili watoto wawili.

Kama ambavyo tumekuwa tukiona kwenye mitandao ya kijamii imekuwa ikisambaa video hiyo ikimuonyesha mwalimu Isaya akiwachapa watoto hao huku pembeni wakiwepo walimu wengine wanne wakicheka na kuonekana kufurahia tukio hilo” Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila akiwaeleza wanahabari.

Amefafanua kwamba tukio hilo likitokea mnamo tarehe 10 January mwaka huu siku moja tuu kuanza kwa kwa masomo ya mwaka wa (2023) ambapo mwalimu huyo aliwaadhibu watoto hao kwa kosa la kutokufanya kazi yake aliyokuwa amewapa kufanyia nyumbani wakati wa likizo.

Ameeleza kuwa kwa mjibu wa ibara ya Elimu namba 24 ya mwaka wa 2002 kuhusu adhabu ya vikobo kwa wanafunzi ni vikobo vinne navyo kwa kuzingatia ukubwa wa kosa, umri, jinsia na afya ya mtoto husika jambo ambalo Isaya alilikiuka na kuwapiga viboko zaidi ya vinne ambavyo aliwachapa maeneo ya nyayo za miguu huku akiwakanyaga miguu yao pia.

Hatua za awali zilizochukuliwa dhidi ya mwalimu huyo ni pamoja na kusimamishwa kazi na kutenguliwa cheo cha ualimu Mkuu na uchunguzi zaidi unaendelea ili kubaini uhakika wa tukio hilo na hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa mara moja ikiwemo ya kumufikisha katika mahakama.

Pamoja na hayo amemuagiza Katibu tawala wa Mkoa Kagera kuchukua hatua za kisheria kwa mratibu elimu kata na kufanyika kwa ukuchunguza zaidi kuhusu ufanisi wa utendaji kazi wa majukumu yake hiyo ikiwa ni sambamba na na kuwachukulia hatua za kinidhamu walimu wale wanaoonekana wakicheka wati likitendeka tukio hilo.

Wanafunzi walichapwa ni Salmoni Kakwezi miaka (9) na Anord kweyamba miaka (10 )wote wanafunzi wa darasa la nne.

Walimu walioonekana wakicheka katika eneo hilo nipamoja na Godson Rwabisho, Beatrce Oswald Kaburanyange, Jemsi Josia, naye Dephina Leonce.

Niwaombe radhi sana watanzania kwa jambo lilitokea la kuumiza na kusisimua kadri tulivyoona alivyopigwa matoto yule alianza kuchechemea tunaamini kabisa moja ya vigezo vinavyopelekea watoto wetu wasiripoti shuleni ni pamoja na adhabu kama hizi zinazokiuka misingi ya haki za binadamu kwa mantiki hiyo tunaendelea kusisitiza kwa walimu wote walezi wote viongozi wote ngazi ya kata kutembelea shule na kufanya vikao vya mara kwa mara na wazazi na walimu lakini zaidi wachukue jukumu la malezi kwa mjibu wa kanuni na taratibu nasema tena niwaombe radhi sana wananchi na wadau wote wa mitandao nchini “Amehitimisha kwa msisitizo huko Mkuu wa Mkoa Chalamila.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!