Home Kitaifa MWALIMU DINNA KANZA AIBUKA KIDEDEA KUWA MWENYEKITI KITENGO CHA WAALIMU WANAWAKE

MWALIMU DINNA KANZA AIBUKA KIDEDEA KUWA MWENYEKITI KITENGO CHA WAALIMU WANAWAKE

Na Julieth Mkireri, Mzawa Media Kibaha

MWALIMU wa Shule ya Msingi Mwanalugali Dinna Kanza ameibuka kidedea kuwa Mwenyekiti wa kitengo cha waalimu Wanawake Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani kwa kuchaguliwa kwa Kura 39 katika Uchaguzi uliofanyika Machi 19 ,2025 .

Dinna ambaye awamu iliyopita alikuwa Mjumbe wa Kitengo hicho hivyo aligombea nafasi hiyo akiwa na Rose Sospeter aliyemaliza muda wake pamoja na Grace Kalinga.

Akitangaza matokeo hayo Katibu wa Chama Cha Walimu( CWT) Mkoa wa Pwani Susan Shesha amesema Dinna ameibuka mshindi baada ya kupata kura 39 akifuatiwa na Rose aliyepata kura 21 na Grace kura 10 hivyo kutokana matokeo hayo Dinna anakwenda kuongoza nafasi hiyo kwa miaka mitano ijayo akiwa na mweka hazina Christabela Mihayo, na wajunbe Edda Michael, Sifa Lucas, Grace Shomia na Ester Peter.

Akizungumza katika mkutano huo Katibu Shesha amewataka viongozi waliochaguliwa kutafuta wataalamu watakaowajengea uwezo walimu Ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Pia amewataka viongozi hao kwenda kujenga mshikamano kwa kuwatumikia kwa uadilifu walimu wengine huku akiwahisia waliokosa nafasi kutokihama chama hicho.

Akishukuru baada ya kuchaguliwa Dinna aliahidi kwenda kujenga ushirikiano wa katika uongozi wake katika kuleta maendeleo katika Kitengo na chama Chama cha Waalimu

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!