Home Kitaifa MWAKAGENDE AIPA KONGOLE TTCL KWA MABORESHO YA MIFUMO YA KIDIGITALI

MWAKAGENDE AIPA KONGOLE TTCL KWA MABORESHO YA MIFUMO YA KIDIGITALI

Na Monica sibanda-Dodoma

Muwakilishi wa wanawake mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Sophia Mwakagende amelipongeza shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL kwa maboresho makubwa waliyoyafanya katika kuhudumia umma hasa katika ulimwengu wa kidigitali.

Pongezi hizo amezitoa leo Agosti 06, 2024 Jijini Dodoma mara baada ya kutembelea banda la Shirika hilo lililopo kwenye maonesho ya Nanenane Nzuguni.

Amesema shirika limefanya maboresho makubwa kuendana na wakati uliopo sasa kwani wanawafikishia huduma wananchi mpaka kwenye makazi yao kwa kupitia huduma yao ya fiber Mlangoni.

“Niipongeze sana Serikali chini ya usimamizi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia shirika hili la TCCL Kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika tumeona sasa mtandao wa interneti unapatikana kila sehemu na ukizingatia sasa hivi Dunia ipo kiganjani” amesema.

Amesema maboresho yaliyoafanyika wao kama jicho la pili la serikali wameridhishwa na kuahidi kushirikiana na serikali kuhakikisha mtandao wa TTCL unafika mbali zaidi.

Ameongeza kuwa ufanyaji wa biashara kwa sasa unategemea zaidi mtandao lakini pia kuanza kwa treni ya umeme SGR kunategemea zaidi mtandao haswa katika ukataji wa treni ili kupunguza msululu kwenye madirisha ya kukatia tiketi.

Sambamba na hayo Mwakagenda ametoa rai kwa shirika hilo kuhakikisha wanafukisha huduma ya intaneti kwa shule za sekondari zilizopo vjijini ili kuwasaidia kujifunza.

“Niwaombe TTCL kupeleka huduma hii kwa shule za sekondari zilizopo vijijini wapate huduma hii kwenye maktaba zao na maabara zao ili waweze kujifunza kwa vitendo”, ameongeza Mwakagende.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!