Home Kitaifa MVUA CHANZO CHA UMEME KUZIMA

MVUA CHANZO CHA UMEME KUZIMA

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Doto Biteko amesema mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbili hapa nchini ndio chanzo cha umeme kukatika katika baadhi ya maeneo kutokana na maji kujaa na kusababisha kuzima kwa mitambo ya kufua umeme katika Kituo cha Kidatu kinacho Peleka umeme kwenye Gridi ya Taifa baada ya kujaa maji

Ameyasema hayo mkoani Morogoro alipotembelea kituo hicho cha kufua umeme ambapo amesema Shirika la Umeme TANESCO baada ya kutokea hitilafu hiyo lilianza kuchukua hatua ya kuondoa maji hayo.

Baada ya kutokea hitilafu ya umeme kuanzia saa nane 08:22 usiku tulianza kuchukua hatua kwa kuanza kuyaondoa maji yaliyosababishwa na uwepo wa mvua nyingi hivyo vijana wamefanya kazi kubwa kuanza kufungua mitambo kwani maji yaliingia kwenye hiyo mitambo na kuchanganyikana na oil ya kwenye mitambo hivyo vijana walianza kuifungua na kuisafisha “Dkt.Biteko

Pia Dkt.Biteko amesema hadi sasa baadhi ya maeneo tayari umeme umeanza kurejea hivyo watanzania waondoe wasiwasi kwani tatizo hilo halijatokana na changamoto ya mgao wa umeme

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!