Home Kitaifa MUWASA YATANGAZA ZAWADI KWA WATAKAOFICHUA WEZI WA MAJI

MUWASA YATANGAZA ZAWADI KWA WATAKAOFICHUA WEZI WA MAJI

Na Shomari Binda
-Muwasa

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) imetangaza zawadi kwa wananchi watakaotoa taarifa ya wezi wa maji.

Katika taarifa iliyotolewa na afisa mahusiano wa MUWASA Chiku Joseph amesema zoezi la kuwabaini wezi wa maji limeanza kwa kupita mtaa kwa mtaa.

Amesema licha ya kuanza kupita na kuwabaini lakini pia taarifa rasmi kutoka kwa wananchi zinapokelewa na zawadi kutolewa.

Chiku amesema zawadi ya shilingi laki moja itatolewa kwa mtoa taarifa huku taarifa hizo ikiwa siri.

Amesema kama Luna mtu au watu wanafanya wizi wa maji kuacha mara moja kwani adhabu yake ni faini na kifungo cha zaidi ya mwaka mmoja jela.

Wakati huo huo Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) mhandisi Nicas Mugisha amefanya kikao kazi kilichohusisha menejimenti na wafanyakazi wote kwa ujumla ikiwa ni pamoja na watumishi kutoka kanda ya Mugumu, Tarime na Shirati.

Lengo la kikao hicho ni kupeana taarifa za utendaji kazi, kujengana na kupeana maelekezo ya kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji kwenye maeneo yanayohudumiwa na MUWASA.

Aidha kwenye kikao hicho Mkurugenzi Mhandisi Nicas alitumia nafasi hiyo kugawa kadi za bima ya afya kwa Watumishi wenye mikataba maalum.

Kwa upande wa watumishi walipata fursa ya kuwasilisha hoja, changamoto na ushauri wa kufanya maboresho zaidi ya kuijenga Mamlaka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!