Home Kitaifa MUWASA YAPOKEA BOMBA KUSAMBAZIA MAJI MITAA SABA

MUWASA YAPOKEA BOMBA KUSAMBAZIA MAJI MITAA SABA

Na Shomari Binda-Musoma

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) imepokea bomba kwaajili ya usambazaji maji mitaa 7 ya pembezoni.

Zoezi la upokeaji bomba hizo umefanyika kwenye ofisi za mamlaka hiyo tayari kuendelea kwa mradi huo wa kuwafikishia wananchi maji majumbani.

Bomba hizo ni sehemu ya bomba zitakazolazwa katika mradi wa ujenzi kwa mfumo wa usambazaji maji kwenda katika maeneo mbalimbali ya mitaa ya Kwangwa A, Kwangwa B, Kiara, Songambele, Nyabisarye, Bweri Bukoba na Nyabange iliyokuwa haipatika huduma ya maji katika Manispaa ya Musoma.

Mradi huo unaogharimu takriban shilingi milioni 709,000,000/=, unatekelezwa na Muwasa na kufadhiliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maji.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (Muwasa) Nicas Mugisha, amesema kufika kwa bomba hizo kutapelekea kazi ya usambazaji kuanza mara moja.

Amesema serikali lengo lake ni kumtua mama ndoo kichwani kwa kuhakikisha wananchi wanapata maji jirani na wao kazi yao ni kuhakikisha wanayafikisha kama ilivyokusudiwa.

Nicas amesema kukamilika kwa mradi huo ambao mpaka sasa utekelezaji wake umefikia asilimia 56 kutawezesha mitaa yote ya manispaa ya Musoma kufikiwa na huduma ya maji safi na salama.

Tumepokea bomba kwaajili ya utekelezaji wa mradi na tunakwenda kufanya utekrlezaji mara moja kwenye maeneo kusudiwa ili kuwafikishia wananchi huduma ya maji” amesema Nicas.

Wananchi wa maeneo yanayokusudiwa kufikiwa na mradi huo wameishukuru serikali kwa kuwaona na kuwaondolea adha ya kupata huduma ya maji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!