Home Kitaifa MUWASA YAKUTANA NA WATEJA NA KUTOA ELIMU KILELE WIKI YA HUDUMA KWA...

MUWASA YAKUTANA NA WATEJA NA KUTOA ELIMU KILELE WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

Na Shomari Binda-Musoma

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) imekutana na wateja na kutoa elimu ikiwa ni kilele cha wiki ya huduma kwa wateja.

Moja ya elimu ambayo imetolewa kwa wateja kwenye kikao hicho kolichofanyika kwenye ofisi za mamlaka hiyo ni pamoja na utoaji wa taarifa za uvujaji wa maji.

Akuzungumza na wateja hao wakiwemo wa majumbani, viwandani na taasisi mbalimbali za umma na binafsi,mkurugenzi wa mamlaka hiyo mhandisi Nicas Mugisha amesema MUWASA inawathamini wateja wake na ipo tayari kuwahudumia ikiwa ni pamoja na taarifa wanazozitoa.

Amesema kupitia wiki ya huduma kwa wateja wamewafikia wateja maeneo yao na kuwapa huduma pamoja na kuwarudishia wale waliositishiwa kuwarejeshea bila kufanya malipo ya faini.

Nicas amesema utoaji wa taarifa kutoka kwa wateja zikiwemo za kupasuka kwa mabomba na kupelekea maji kuvuja zinafanyiwa kazi kwa haraka.

Amesema upotevu wa maji kutokana na mivujo na kupasuka kwa mabomba kunatia hasara hivyo kuwaomba wateja kutoa taarifa kila wanapoona hali hiyo.

Aidha Nicas amesema mamlaka imekuwa ikitoa ” bili” kwa wakati kupitia simu za mkononi na kuwataka wateja wazilipie kwa muda muafaka ili kuepuka kusitishiwa huduma ya maji na kuingia kwenye faini.

Wakizungumza kwenye kikao hicho wateja kwa upande wao wameishukuru mamlaka hiyo kwa huduma nzuri wanazozitoa na kufika kwa wateja kwa wakati mara baada ya kupokea taarifa.

Katika wiki ya huduma kwa wateja MUWASA imeitumia kuwasikiliza wateja na kuwarudishia huduma ya maji wale waliokuwa wamesitishiwa bila kufanya malipo ya faini zoezi ambalo bado linaendelea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!