Home Kitaifa MUSOMA VIJIJINI WAUNGANA KUPONGEZA AZIMIO LA RAIS SAMIA KUGOMBEA 2025

MUSOMA VIJIJINI WAUNGANA KUPONGEZA AZIMIO LA RAIS SAMIA KUGOMBEA 2025

Na Shomari Binda_Musoma

WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Musoma vijijini wamesafiri hadi Musoma mjini kupongeza azimio la Mkutano Mkuu wa chama hicho kumpitisha Rais Samia kugombea uchaguzi wa 2025.

Wakizungumza kwenye viwanja vya Mara sekondari wakati wa kuunga mkono azimio hilo baada ya maandamano ya amani yaliyoandaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM mkoa wa Mara(UVCCM) wamesema wamelipokea kwa dhati azimio hilo.

Wamesema kwa mambo makubwa ambayo yamefanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan hawana budi kuunga mkono azimio hilo.

Diwani wa Kata ya Nyakatende Majira Mchele amesema kwa Musoma Vijijini Rais Dkt.Samia amewafanyia mengi mazuri ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na kuwapa fedha nyingi kwaaǰili ya miradi ya maendeleo

Amesema walikuwa Hawana hospital tangu nchi ipate uhuru lakini kwa sasa wana hospital ya Wilaya, vituo vya afya na zahanati zinazotoa huduma za afya kwa wananchi.

Majira amesema kwenye sekta ya elimu miundombinu ya elimu imejengwa na kuwezesha wanafunzi kutoka kusomea chini ya miti na kusomea kwenye madarasa mazuri na kukaa kwenye madawati .

Kuhusu maji diwani huyo amesema miradi ya maji Imeendelea kusambazwa Jimbo la Musoma vijijini na kumtua mama ndoo kichwani maeneo mengi.

Tumefika hapa Musoma mjini kuungana na wana CCM mkoa wa Mara kupongeza azimio la Mkutano Mkuu la kumpitisha Mwenyekiti wetu wa Taifa Rais Dkt Samia kugombea uchaguzi wa mwaka 2025.

Jimbo la Musoma vijijini tumefanyiwa mambo makubwa na Rais Samia ndio maana tumesafiri hadi Musoma kuunga mkono azimio”, amesema.

Aidha diwani huyo na wanachama kutoka Kata ya Etaro, Nyakatende na maeneo mengine ya jimbo la Musoma vijijini amemshukuru mbunge wa jimbo la Musoma vijijini profesa Sospeter Muhongo kwa kutoa usafiri na fedha ya chakula kwenye tukio hilo.

Wamesema licha ya taarifa ya muda mfupi lakini mbunge huyo amewawezesha kujumuika na kuungana kupongeza azimio hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!