Desemba 31 , 2023 Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro amehitimisha rasmi Mbio za Riadha zilizoandaliwa na Umoja wa Nchi za India na Tanzania ambazo zimekua zikiendelea kuanzia hapo Jana Desemba 30 Umbali wa Km 120 Dar Es Salaam – Bagamoyo – Dar Es Salaam na kuhudhuriwa na wakimbiaji mbalimbali kutoka hapa Nchini Tanzania na India akiwemo Mwanariadha Mkongwe na Muigizaji Maarufu wa Filamu za Kihindi Bwn. Milind Sowman.
Aidha Waziri Ndumbaro amesema Mbio hizi kufanyika Nchini Tanzania ni matokeo ya Uhusiano Mzuri kati ya Tanzania na India na Matokeo ya Ziara ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Nchini India aliyoifanya mapema Oktoba 2023.
” Naomba nitoe Shukran kwa Mhe Balozi wa India hapa Nchini Binaya Srikanta Pradhan kwa kulifanikisha hili , Kwa maana Oktoba Mwaka huu Rais Samia katika ziara yake Nchini India alishuhudia utiaji Saini wa Mikataba Miwili ambayo ni Mkataba wa Ushirikiano wa Miaka Mitano ya Ushirikiano katika Masuala ya Utamaduni kati ya Tanzania na INDIA na Mkataba wa Ushirikiano wa Muda mrefu katika Masuala ya Michezo, Mikataba hii Miwili sisi kama wizara tunaenda kuitekeleza ipasavyo na utekelezaji wake umeanzia katika mbio hizi Muhimu ambazo tunaahidi zitakua zikiendelea mwaka hadi mwaka” amesema Waziri
Aidha Waziri Ndumbaro amesema mbio hizi kwa Mwaka wa 2024 zitafanyika kwa mara ya pili Nchini katika Hifadhi ya Taifa ya KITULO wiki ya kwanza ya Mwezi Julai, ili wakimbiaji wa Wageni wote waweze kujionea upekee wa Hifadhi hii iliyojawa Maua, Ndege, na Wanyama Rafiki ambayo vitaifanya Marathon hii kuwa ya kipekee Duniani.
Aidha Bwn. Sowman ambaye aliambatana na Mkewe , pamoja na Mama yake Mwenye Umri wa Miaka 75+ ambaye nae ameshiriki mbio hizi, amewapongeza wanariadha wa Tanzania kwa Ushiriki wao katika mbio hizo na kuahidi kurudi tena Tanzania kushiriki mbio hizi hizi zinazotarajiwa kufanyika tena Julai 2024 katika Hifadhi ya Taifa ya KITULO.
Kwa upande Mwingine Msajili wa Vyama vya Michezo Nchini Bwn. Evordy Eliezer Kyando ameahidi kuhakikisha wanatekeleza maelekezo yote ya Wizara na kuziendeleza mbio hizi ambazo zinalenga kuimarisha Utalii, Urafiki wa Tanzania na INDIA na Kuboresha Mahusiano ya Wataalam wa Sekta ya Riadha , Filamu na Kuogelea kutoka katika nchi hizi mbili.