Home Kitaifa MUIGIZAJI GABO ZIGAMBA ALAMBA DILI NONO KIBOKO PAINTS , SOMA HAPA MAAJABU...

MUIGIZAJI GABO ZIGAMBA ALAMBA DILI NONO KIBOKO PAINTS , SOMA HAPA MAAJABU YA KIBOKO WALL PUTTY

Baadhi ya Mafundi kutoka maeneo ya Buguruni Jijini Dar Es Salaam katika semina iliyoandaliwa na kampuni ya Uuzaji wa Vifaa vya Ujenzi nchini ya KIBOKO PAINTS ambapo kampuni hiyo imetambulisha bidhaa yake mpya ya KIBOKO WALL PUTTY kwa mafundi hawa , sambamba na hilo KIBOKO PAINTS imemtambulisha Muigizaji Gabo Zigamba ( wa tatu kutoka kushoto kwa waliosimama )  kama Balozi wake, utambulisho uliofanywa na Afisa Masoko Mkuu wa Kampuni ya KIBOKO PAINTS Bwn. Erhard Mlyansi ( aliyevaa Tisheti Nyekundu ) , Leo June 22 , 2024.

Mmoja wa Mafundi akiifanyia majaribio kwa kuipaka ubaoni bidhaa ya KIBOKO WALL PUTTY  mbele ya mafundi wenzake ili kuwathibitishia ubora wake katika semina iliyofanyika Buguruni Jijini Dar Es Salaam ( kulia ni Bwn. Amani Nduli kutoka kampuni ya KIBOKO PAINTS na kushoto ni Bwn. Hamidu ambaye ni Afisa Mauzo )

Na Adery Masta. 

Kampuni namba moja nchini kwa uuzaji wa Vifaa mbalimbali vya Ujenzi kama vile Mabati , Rangi n.k  KIBOKO Paints, Imetambulisha Bidhaa yake mpya sokoni ya KIBOKO WALL PUTTY yenye Ubora wa hali ya juu kwa baadhi ya Mafundi Rangi wanaoishi na kufanya kazi karibu na eneo la Buguruni  Jijini Dar Es Salaam.

Hayo yamebainishwa Leo , April 27, 2024 katika Semina iliyotolewa na Kampuni ya KIBOKO PAINTS kwa Mafundi Rangi wa Buguruni na maeneo jirani.

Akizungumza baada ya Semina , Bwn. Hamidu ambaye ni Afisa Mauzo wa kampuni, lakini pia Mkufunzi wa Semina hiyo amesema 

Kampuni ya KIBOKO PAINTS inafanya Semina hizi nchi nzima ambapo kwa upande wa Dar Es Salaam imeshafanyika Gongo la Mboto na maeneo yake ya karibu , Buguruni na maeneo yake ya karibu , Mbezi na hatimae Kariakoo . 

” Tunaendelea na Semina hii kwa Mafundi huku tukitambulisha Bidhaa yetu Bora kabisa sokoni ya KIBOKO WALL PUTTY ambayo imepokelewa na kupendwa na Mafundi kutokana na Ubora wake , KIBOKO WALL PUTTY inaweza kutumika Nje , Ndani , Kufungia Mikanda na Dari , ni nyeupe na inaweza kufanya ukuta wako kung’ara hata kama haujapigwa rangi ”  amesema Bw. Hamidu

Anton Thomas ni fundi rangi aliyezungumza na Mwandishi Wetu Baada ya Semina hiyo ameipongeza kampuni ya KIBOKO PAINTS kwa kuileta sokoni KIBOKO WALL PUTTY yenye Ubora wa hali ya juu 

“KIBOKO WALL PUTTY ni Bora sana ukiitumia hutopata gharama ya kununua material mengine tofauti ya kufanya Skimming , KIBOKO PAINTS wamefanya maboresho makubwa na kuja na Wall putty Bora kuliko nyingine zilizopo sokoni “ amesema.

Aidha KIBOKO PAINTS imemtambulisha Muigizaji Gabo Zigamba kama Balozi wake,  Muigizaji huyo ameahidi kufanya makubwa ili kuzitangaza bidhaa za KIBOKO.

.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!