Home Kitaifa MUHONGO KUENDESHA HARAMBEE UJENZI WA SEKONDARI 4 JIMBONI

MUHONGO KUENDESHA HARAMBEE UJENZI WA SEKONDARI 4 JIMBONI

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini,Prof.Sospeter Muhongo, amepanga kuendesha harambee kufanikisha ujenzi wa sekondari 4 kwenye jimbo hilo.

Akizungumza na Mzawa amesema ndani ya jimbo kwa sasa kuna ujenzi wa sekondari 4 ambao unaendelea na kutarajiwa kufunguliwa januari mwakani.

Amesema jumla ya shule za sekondari zilizopo kwa sasa ni 27 za serikali zikiwa 25 na binafsi 2 huku jimbo likiwa na vijiji 68 ambapo sekondari zinapaswa kuongezeka.

Muhongo amesema amepanga kuanza ziara ya kuzitembelea Kata zinazoendelea na ujenzi na kuendesha harambee.

Amesema viongozi wa maeneo ya ujenzi wanapaswa kuwaandaa wadau mbalimbali ili waweze kushitiki harambee hizo na kukamilisha ujenzi kwa wakati.

Amevitaja Vijiji vinavyojenga sekondari mpya zitakazofunguliwa januari 2024 kuwa ni Nyasaungu Kata ya Ifulifu, Muhoji
Kata ya Bugwema, Wanyere Kata ya Suguti,pamoja na kisiwa cha Rukuba Kata ya Etaro.

Aidha katika ziara hiyo mbunge huyo ataongea na wananchi kuzungumzia juu ya umuhimu wa elimu kwa wakati wa sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!