Home Kitaifa MUHONGO ASISITIZA KILA KIJIJI KUWA NA SHULE YA MSINGI NA SEKONDARI JIMBO...

MUHONGO ASISITIZA KILA KIJIJI KUWA NA SHULE YA MSINGI NA SEKONDARI JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema lengo ni kuhakikisha kila Kijiji na Kitongoji kinakuwa na shule ya msingi na sekondari ndani ya jimbo.

Kauli hiyo ameitoa mapema leo jumapili januari 5 akikusudia Musoma Vijijini ya leo na kesho katika suala la elimu na mengine.

Amesema hayo yote hayawezi kukamilishwa kwa mwaka mmoja na kuishukuru serikali kwa kuunga mkono jitihada hizo.

Muhongo amesema kila Kijiji kinapaswa kuwa na shule ya msingi zaidi ya moja kutokana na wingi wa watoto ambapo kwa sasa zipo shule 120 za serikali zikiwa 116 za binafsi 4.

Amesema kila sekondari inapaswa kuwa na maabara tatu za masomo ya sayansi ambayo yatawawezesha wanafunzi kuingia kwenye soko la ushindani

Licha ya mkazo kwenye elimu amezungumzia pia suala la afya na kudai kila Kijiji kuwa na zahanati itakayotoa huduma karibu na wananchi.

“Ndugu zangu naendelea kuwathibitishia kwamba tunajua tunakoelekea hatufanyi kazi kwa kubahatisha wala kwa msimu Malengo yetu yanatekelezwa na serikali yetu inachangia na kutuunga mkono sana.

Musoma Vijijini ya leo na ijayo kila kijiji kuwa na shule za msingi zaidi ya moja kulingana na wingi wa watoto na haya yote ynafanyika kwa muda”,amesema.

Amesema suala la umeme na maji kila Kijiji na Kitongoji yanakwenda vizuri ambapo itawezesha kilimo cha umwagiliaji kwenye mabonde ya Bugwema na Suguti.

Mbunge huyo amezungumzia pia suala la uvuvi wa vizimba kuimalishwa katika kuinua uchumi na kuhakikisha barabara zinapitika wakati wote wa masika na kiangazi huku mawasiliano ya simu yakipatikana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!