Home Kitaifa MUHONGO AKAGUA KUANZA MRADI WA MAJI MUGANGO-TEGERUKA

MUHONGO AKAGUA KUANZA MRADI WA MAJI MUGANGO-TEGERUKA

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa jimbo la Musoma vijijini Prof. Sospeter Muhongo amesema wananchi wa vijiji vya Kata za Mugango na Tegeruka wanayo matumaini makubwa ya kupata huduma ya maji.

Matumaini hayo yamekuja baada ya kuanza kuchimbwa mitaro yenye utefu wa kilometa 15 kwaajili ya usambazaji wa mabombo hayo.

Muhongo ameyasema hayo alipotembelea kuona maendeleo ya mradi huo unaoghalimu kiasi cha shilingi bilioni 4.75 katika vijiji vya Msyani na Tegeruka.

Amesema kazi kuendelea kwa kasi na baadhi ya vifaa kuwasili eneo la tukio kumekuwa na matumaini makubwa kwa wananchi.

Mbunge huyo amewataka vijana wanaoshiriki mradi huo kufanya kazi kwa weledi na kulinda miundombinu ili ikamilike kwa wakati uliokusudiwa.

Amesema Kata 4 zenye jumla ya Vijiji 12 za jimbo la Musoma Vijijini zina miradi ya kusambaziwa maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria.

Mradi wa Bomba kuu la maji la Mugango- Kiabakari lina gharama ya shilingi bilioni 70.5
na lina uwezo wa uzalishaj wa lita milioni 35 kwa siku na mitambo ya kusukuma maji inayotengenezwa China, Hungary na Turkey italetwa nchini hivi karibuni”

Tenki lenye ujazo wa lita 135,000 linajengwa Kijijini Kataryo,jili tenki litapokea maji kutoka kwenye Tenki la Kijijini Kiabakari lenye ujazo wa Lita milioni 4 hii yoye ni kufikisha maji kwa wananchi” ,amesema Muhongo.

Wananchi wa jimbo la Musoma Vijijini wanaishukuru serikali chini ya uongozi mzuri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji ya bomba vijijini mwetu. Kila kijiji kinao mradi wa maji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!