Home Kitaifa MUHONGO ACHANGIA VITI 200 KWANYE UMOJA WA JAMII YA WATU WA MUSOMA...

MUHONGO ACHANGIA VITI 200 KWANYE UMOJA WA JAMII YA WATU WA MUSOMA KWAAJILI YA HUDUMA ZA KIJAMII

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amechangia viti 200 vyenye thamani ya shilingi milioni 4 kwa umoja wa jamii ya watu wa Musoma.

Viti hivyo vimetolewa na mbunge huyo kwaajili ya kusaidia umoja kwenye matukio ya kukutana ikiwa ni kwenye misiba,sherehe na masuala mengine ya kijamii.

Wakizungumza na Mzawa Blog mjini hapa leo februari 23 wana umoja wa jamii ya watu wa Musoma wamemshukuru mbunge huyo kwa moyo wake wa upendo na kuwachangia viti hivyo.

Wamesema wamekuwa wakiangaika kukodisha viti na kutumia fedha nyingi wanapokutwa na matukio na kupatikana kwa viti hivyo ni msaada na mchango mkubwa kwao.

Mmoja wa wana jamii hao Ibrahim Assey amesema Muhongo ni mbunge wa kuigwa katika kuchangia shughuli na makundi ya kijamii.

Amesema walikuwa na mahitaji ya viti na vifaa vingine kwaajili ya umoja na kwa kuanzia tayari wamepata viti na uongozi unaendelea na upatikanaji wa vifaa vingine ikiwa ni pamoja na tenti na vyombo vya muziki.

” Tunamshukuru sana mheshimiwa Muhongo kwa mchango wake wa viti kwenye umoja wa jamii ya wana Musoma ambavyo vimekuja kwa muda muafaka.

” Viti 200 ni mchango mkubwa kutoka kwake lakini tunawashukuru pia wana umoja wenyewe kwa kuchangia pamoja na wachangiaji wengine”,amesema.

Akizungumzia uchangiaji wa viti ulivyokwenda mara baada ya hafla iliyofanyika februari 21 Mwenyekiti wa umoja wa jamii ya wana Musoma Benedict Magiri amesema viti 600 vilipatikana na zaidi ya fedha taslimu zaidi ya milioni 3 katika tukio hilo.

Magiri pia amemshukuru mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo kwa mchango wake mkubwa pamoja na wachangiaji wengine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!