Home Kitaifa MUHEZA KWANZA WAPIGA JEKI VIFAA VYAKUJIFUNGULIA VITUO VYA AFYA MUHEZA

MUHEZA KWANZA WAPIGA JEKI VIFAA VYAKUJIFUNGULIA VITUO VYA AFYA MUHEZA

Na Boniface Gideon, MUHEZA

Shirika lisilo la kiserikali la Muheza kwanza mwishoni mwa wiki limetoa msaada wa vifaa vya kujifungulia kwa akina mama zaidi ya 200 katika vituo vya Afya Mkuzi na Ubwari vilivyopo wilayani humo. Msaada huo ni sehemu ya mpango kazi wa Shirika hilo wakuisadia Jamii katika Sekta za Afya, Elimu, Maji pamoja na uwezeshaji wa kijamii.

Akikabidhi msaada huo Jana, Mkurugenzi wa Muheza kwanza Hamis Rajab alisema Shirika hilo linaundwa na wakazi wa Wilaya ya Muheza wanaoishi nje ya Wilaya hiyo.

Sisi ni wazaliwa wa Muheza tunaoishi nje ya Wilaya yetu na wengine wapo nje ya Nchi, tumejiunda na kuwa Shirika lengo letu ni kwa ajili yakuibadilisha kimaendeleo Wilaya yetu, tumeunda Shirika letu la Muheza kwanza kwa ajili yakuisadia Serikali kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi wa Muheza” Alisema Hamis

Alisema vifaa hivyo vyakujifungulia vitawawezesha akinamama zaidi ya mia mbili kupata huduma yakujifungua bila changamoto kubwa.

“Sote tunafahamu kuwa Serikali yetu inapambana kuboresha huduma za Afya hususani Afya ya Mama na Mtoto lakini kupitia vifaa hivi tunaamini vitaenda kuongezea palipopungua na kuwawezesha akinamama wajawazito kujifungua Salama kabisa” alisema Hamis

Alisema wataendelea kusaidia katika kuboresha huduma za Afya, Elimu, Maji pamoja na uwezeshaji wa kijamii.

“Huu ni mwanzo tu wa mpango kazi wetu kwa Wilaya yetu ya Muheza,bado tunamambo mengi yakufanya hususani kwenye Sekta za Afya, Elimu, Maji pamoja na uwezeshaji wa kijamii, tutaendelea kushirikiana na Serikali yetu katika kupunguza changamoto kubwa zinazowakabili Wananchi wa Muheza” alisema Hamis

Akipokea msaada huo,Ofisa utawala ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo Nelson kasiki alilishukuru Shirika hilo kwa msaada huo,
“Niwashukuru sana Muheza kwanza kwa msaada huu ambao utaenda kuwasaidia akinamama kujifungua Salama, lakini pia niwapongeze kwakujiunda na kutengeneza Shirika ili kuwasaidia wananchi wa Muheza ni jambo zuri na lakuigwa, niwaombe wadau wengine nao wajitokeze kusaidia zaidi ya hapa ,bado Jamii yetu inauhitaji mkubwa wa huduma muhimu za kibinadamu” Alisema Nelson

Aliwataka wahudumu wa Afya kufanya kazi kwa weledi kwakufuata miongozo ya Afya na kujiepusha na tabia zinachafua sifa ya huduma za Afya,

“Kwa siku za hivi karibuni tumekuwa tukisikia na taarifa kupitia vyombo vya habari wahudumu wa Afya kukengeuka, niwaombe wahudumu wa Afya acheni kutoa lugha chafu kwa akina mama hususani wajawazito, pia vifaa hivi vikatumike kama watoaji walivyolenga, msije mkaenda kuviuza “Alisema Nelson

               MWISHO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!