Home Kitaifa MTEMVU AKABIDHI HELMETS NA REFLECTOR KWA BODABODA KIJITONYAMA

MTEMVU AKABIDHI HELMETS NA REFLECTOR KWA BODABODA KIJITONYAMA

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam Comred Abbas Mtemvu amewataka wanachama wa CCM kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwa wanaCCM ili CCM iendelee kushinda katika chaguzi 2024/ 25.

Mwenyekiti huyo ameyasema hayo kwenye hafla fupi ya kukabidhi helmets na reflector kwa Dereva Bodaboda wa Tawi la Bwawani Kata ya Kijitonyama wikayani Kinondoni mkoani Dar es salaam ambapo pia zoezi la kuwapokea wanachama wapya wa kasi za kisasa za CCM.

Amesema CCM mkoa wa Dar es salaam imepokea kadi zaidi ya elfu 20 ili kuwakabidhi wanachama hao wakati wanasubiri awamu nyingine ya kupokea kadi hizo ambazo zinaendelea kuboreshwa na Makao makuu ya Chama.

Akielezea suala la makundi ndani ya Chama amewataka wanachama kuwaacha viongozi waliopo madarakani wafanye kazi zao hadi muda wao utapomalizika ndipo wengine wajitokeze ila kwa sasa kuwaingilia waliopo ni kuwaondoa katika reli na mipango ya kuwatumikia na kuanza kujibu mapigo wakati maendeleo yanasimama.

Amesema kwa kuwa Siasa ni maisha yeyeto anayeshabikia mtu anayecheza na siasa na kuleta ushabiki anafanya jambo la hatari kwani CCM inamkakati wa kuinua Maisha ya watanzania kuyaboresha.

Hatahivyo Mwenyekiti wa Tawi la CCM Bwawani Kata ya Kijitonyama Twaha John amesema alikutana Wadau wake ambao walimpa helmets hizo na reflector kwaajili ya vijana wa Bodaboda wa Tawi la Bwawani.

Amesema anafanya hivyo kwa Nia ya dhati ya kuwasaidia vijana wenzake ambapo wiki iliyopita pia alikabidhi jezi za michezo kwa timu ya chipukizi wa CCM na timu ya mpira ya Tawi la Bwawani.
++++++++++++++

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!