Home Kitaifa MSTAHIKI MEYA KUMBILAMOTO: TUMIENI MITANDAO KUFANYA BIASHARA DUNIA IKO KIGANJANI

MSTAHIKI MEYA KUMBILAMOTO: TUMIENI MITANDAO KUFANYA BIASHARA DUNIA IKO KIGANJANI

Na Magrethy Katengu —Dar es salaam

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omar Kumbilamoto amewaasa wafanyabiashara kufanya biashara kwa kutumia mitandao ikiwa na lengo kukuza biashara zao kwani kwa sasa zinapatikana hadi za mkopo ni Uaminifu tu wa kulipa.

Ameyasema hayo leo Mei 2, 2024 wakati alipokuwa akizindua duka la simu la Mandasi Store lililopo Banana jijini Dar es Salaam ambapo amebainisha kuwa aliyeamua kufanya biashara hiyo ya simu aliangalia mahitaji ya soko hivyo akaamua kusogeza karibu na jamii kwa kuwauzia kwa gharama nafuu sawa na bei ya sokoni kariakoo huku akikopesha wale ambao hawana uwezo wa kulipa keshi kwani ametambua kuwa siku zote watu hawafanani vipato vinatofautiana.

“Niseme kuwa ninaona furaha kuona kijana kama huyu anaamua kujiajiri na kuzalisha ajira kwa vijana wengi kupitia ubunifu wake huu hivyo nawasisitiza mnapokopa simu kuweni waaminifu kulipa msisumbue wafanyabiashara njoeni na vitambulisho vya NIDA na kianzio baadhi ya simu ila simu nyingine zinamuhitaji mtumishi wa umma ni gharama kubwa atakatwa kwenye mchahara wake” amesema Meya

Kumbilamoto amesema kuwa dunia ya sasa inahitaji mfanyabiashara kutumia mawasiliano ikiwa kama sehemu kuwafikia wateja kwa urahisi ambapo kwa kufanya hivyo kutaweza kutangaza biashara husika na hatimaye kukuza na mitaji yao na hatimaye kulipa kodi kwa nchi ambayo inaleta maendeleo kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi Mtendaji Mandasi store mduka ya simu hilo, Abdulah Omar Juma amesema kwa sasa wao wanalenga kuwawezesha Wananchi wote kumiliki simu kwa gharama nafuu ikiwa pamoja na kuwakopesha kwa utaratibu wa kulipa kidogo kidogo kwa muda watakao kubaliana mteja atapewa utaratibu na hatimaye kulipa kwa urahisi bila usumbufu wowote, hivyo Wananchi wote wanakaribishwa kwenye duka hilo ili kujipatia simu bora na za kijanja.

Kampuni ya mandasi imeweza kuwasaidia wananchi elfu ishirini na sita kwa kuwakopesha simu wakilipa kidogo kidogo na sasa wana matawi yapatayo 14, ya maduka katika mikoa 10, Tanzania nzima na tumeweza kuajiri vijana 36

Aidha wito umetolewa kwa baadhi ya watu kuacha tabia mbaya kutumia mitandao kinyume na utaratibu jambo linalopelekea mmong’onyoko wa maadili kwa vijana wengi na watoto.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!