Na Magreth Mbinga
Mkazi wa Lindi Hamidu Mohammed Abdallah(28) leo Januari 4 ,2023 amekabidhiwa rasmi gari yake aina ya Toyota Urban Cruiser yenye thamani ya Sh Milioni 65 baada ya kuibuka mshindi wa promosheni ya Chomoka na ndinga kutoka Parimatch.
Promosheni hiyo iliyodumu kwa muda wa siku 35 kuanzia Novemba 22 hadi Disemba 26 ,2022 iliwapa wateja nafasi za kujishindia zawadi za simu mbili kila siku ,bodaboda kila mwisho wa wiki na droo ya mwisho mshindi alikuwa akijishindia gari mpya kabisa .
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa kampuni ya Parimatch Tanzania,Bwana Erick Gerald wakati wa kukabidhi gari hilo kwa mshindi na kuwashukuru wateja wote ambao wameshiriki na baadhi yao kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo simu na bodaboda ambazo zilitolewa na kampuni hiyo.
“Tunayo furaha kubwa katika kipindi hiki cha mwaka mpya kimkabidhi mshindi wetu wa gari ya aina Toyota Urban Cruiser,gari hili ni jipya kabisa yaani zero Kilometa ,tunawashukuru wateja wetu Nchi nzima walioshiriki kwenye promosheni hii ya siku 35 ambayo imemalizika mwishoni mwa mwezi Disemba 2022″amesema Gerald.
Kwa upande wake mshindi wa gari hiyo ,Hamidu Mohammed amewashukuru Parimatch Tanzania kwa kuweza kutimiza ndoto yake kumiliki gari kutoka katika kampeni ya Chomoka na ndinga.
“Wakati napigiwa simu nilikuwa nyumbani nimelala siku hiyo kulikuwa na mvua kubwa ,sikuweza kuamini kwa haraka Ila baadae nilipopigiwa tena na kupata taarifa kwamba nimeibuka mshindi nilifurahi sana kwani sikutegemea kabisa kuwa ningeibuka mshindi katika promosheni hii ,jambo hili naliona kama ndoto kwangu”amesema Hamidu.
Aidha Afisa Mauzo wa kampuni ya Toyota Shamim Omary amesema wameungana na Parimatch kutoa gari hiyo mpya aina ya Urban Cruiser ambayo Ina cc 1500 pia inaulaji mzuri wa mafuta ikiwa ni toleo jipya kabisa la 2022 inabeba watu 5 na ipo juu.
“Tuliangalia gari ambayo itaweza kumfata Mtanzania yeyote kwamba ataweza kuimudu kwenye shughuli zake za kila siku kama anafamilia itamfaa hata asiye na familia ambapo ataweza kuifanyia biashara au kwa matumizi yake binafsi “amesema Shamim.