Home Kitaifa MSD YA TANZANIA YAVUTIA SIERRA LEONE KUJA KUJIFUNZA NAMNA YA UTOAJI HUDUMA...

MSD YA TANZANIA YAVUTIA SIERRA LEONE KUJA KUJIFUNZA NAMNA YA UTOAJI HUDUMA BORA NCHINI KWAO

Na Magrethy Katengu—Dar es salaam

Bohari ya Dawa Nchini Tanzania (MSD) imepokea ujumbe kutoka Bohari ya Dawa ya Sierra leone uliokuja kujifunza namna ya kuboresha mifumo ya utoaji wa huduma ya dawa nchini kwao .

Akizungumza Aprili 29 ,2024 mara baada ya Ujumbe huo kuwasili nakufanya mazungumzo na Wataalamu wa MSD,Mkurugenzi wa huduma za dawa na Mfamasia Mkuu wa Serikali .Daud Msasi …amesema kuwa Bohari ya Dawa ya Seirra Leone na Bohari ya Dawa nchini Tanzania ( MSD) kupitia ujio huo utaleta tija ya ushirikiano na utaongeza fursa ya kibiashara kwa kuendelea kujinadi bidhaa wanazozalisha katika sekta ya Dawa .

Sanjari na hayo amebainisha kuwa Seirra Leone imeichagua Tanzania kua kituo cha kujifunzia mifumo ya utoaji wa huduma ya dawa kwa wananchi wake kutokana na mageuzi makubwa yaliyofanywa serikali ya Tanzania katika Sekta ya Dawa baada ya kuanzisha kampuni tanzu ya utengenezaji na uagizaji wa dawa,Vifaa tiba na Vitendanishi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo Global Fund, UNFPA

“Andiko lao wamepeleka nchi nyingi za Afrika na walipokaa na kuanza kuchambua ni nchi , wamegundua Tanzania ni Nchi nzuri kwa kujifunzia kupitia MSD, sasa tutawapa ushirikiano kwani wanataka kujifunza namna ya mifumo ya utoaji wa huduma kwa wananchi wa bara la afrika kwa ujumla” amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Maverre Tukai amebainisha kuwa Sierra Leone wameamka upya mara baada ya kuvunjavunja MSD yao kutokana na machafuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe hivyo wana miaka sita na wanataka waendeshe huduma kwa kasi hivyo wmekuja kujifunza kwani sisi kuna vitu vingi tunafanana ikiwemo manunuzi, hivyo wamevutiwa sana na uhimivu ,matumizi ya tehama, kununua bidhaa kwa niaba ya wafadhi kwa kweli wamefurahi sanaa kuona namna MSD inavyofanya kazi.

“Tanzania tuko vizuri wametuomba tushirikiane sana kubadilishana uzoefu baina ya wataalam wetu na wataalamu wao ili wafahamu vitu vingi zaidi ikiwemo kampuni tanzu ambayo kwao haipo nasisi tutajitahidi kuwa karibu nao kwani tunashabiiana baadhi ya mifumo ya wizara ya afya” amesema Maverre

Nae Mkurugenzi wa huduma za Dawa na Mfamasia Mkuu Serra Leone Moses Batema amesema baada ya nchi hiyo kukumbwa na machafuko ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ilipelekea taasisi nyingi za nchi hiyo kuvunjika ikiwemo Bohari ya Dawa ya nchi hivyo kwasasa imeanzishwa upya ambapo mpaka sasa ina miaka sita tangu kuanzishwa kwake na nia yao ni kuiendesha vizuri isiyumbeyumbe kiuendeshaji iwe imara kama MSD ya Tanzania.

“Ziara hii tumekuja MSD kujifunza namna taasisi hii inavyojiendesha bila kutetereka kifedha, kiutendaji, tumejionea na kujifunza ubunifu mkubwa unaofanywa na wenzetu( MSD) hivyo tutashirikiana kwa ukaribu zaidi kupitia wataalamu wetu kwa kufundisha ujuzi wa mifumo mbalimbali ikiwemo ununuzi na usambazaji wa dawa, na vifaa tiba” amesema Dkt Katema

Vilevile Mkurugenzi Kaimu Naibu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Uendeshaji Bohari ya Dawa ya Sierra Leone Jatu Abdulai ameishukuru menejiment ya MSD kwa kuonesha ushirikiano mzuri huku akiwa na matumaini makubwa ya Bohari ya Dawa ya nchi yake kupata mafanikiao makubwa kupitia ushirikiano huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!