Home Burudani BEN POL AACHIA KIBAO CHA KUFUNGIA MWAKA 

BEN POL AACHIA KIBAO CHA KUFUNGIA MWAKA 

MSANII nguli wa Muziki wa R&B  hapa nchini Behnam Paul maarufu kama Ben Pol ameachia kibao kipya kinachofahamika kama Nyumbani. 

Katika wimbo wa Nyumbani Ben Pol ambaye asili yake ni Dodoma ameeleza raha na uzuri wa kurejea Nyumbani huku akisifia maadili mazuri, mtindo wa maisha, vyakula n.k katika jamii zetu za kitanzania.

“Kwangu mimi Nyumbani ni zaidi ya sehemu tu, Nyumbani ni mahali popote ambapo unahisi upendo na amani, unajihisi kupata sapoti, unasikilizwa, unaeleweka, unapokelewa katika hali zote bila kujali mafanikio yanayoonekana kwa macho.

Nawakaribisha wadau wote wa Muziki wa Tanzania kufurahia wimbo huu ambao sasa unapatikana katika mitandao yote tukiendelea kujivunia tulikotoka, kujivunia utanzania wetu, u-Afrika wetu, utu wetu” – Ben Pol.

Video ya Nyumbani imefanyika katika mikoa ya Dar es salaam na Pwani chini ya utayarishaji wa kampuni ya Redshot.

….Mwisho..

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!