Mkurugenzi wa Msama Promotions Alex Msama ametoa ufafanuzi wa suala la umiliki wa kiwanja plot namba moja block No DSMT 1022673 kilichopo Kigamboni Kibada mji Mwema baada ya Waziri wa Ardhi Jerry Slaa kudai kuwa amekivamia kiwanja hicho .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Msama amesema kiwanja hicho ni chake anaumiliki halali na hajawai kuwa tapeli wa kiwanja cha mtu yoyote.
“Kiwanja ninakimiliki kwa halali na nimemilikishwa na Wizara ya Ardhi kwa halali na tuhuma za kumiliki kiwanja bweni sijawai kumiliki kiwanja cha bweni sio changu na sikijui sina taarifa nacho.”
“Nimesikitishwa na Diwani wa Kigamboni wa Kibada aliyempa Waziri taarifa za uongo kuwa nimewatapeli wananchi sio kweli ninamiliki kwa halali.”amesema Msama