Home Kitaifa MRADI WA TIGO eSchools WAIFIKIA BENJAMIN MKAPA SEKONDARI

MRADI WA TIGO eSchools WAIFIKIA BENJAMIN MKAPA SEKONDARI

Viongozi mbalimbali kutoka kampuni ya Tigo akiwemo Afisa Mtendaji Mkuu Bwn. Kamal Okba , katika picha ya pamoja na Uongozi wa Shule ya Sekondari BENJAMIN MKAPA mapema leo hii Tigo walipoitembelea shule hiyo kwa ajili ya kujionea jinsi gani walimu na wanafunzi wanavyonufaika na mradi wa Tigo e-School unaotekelezwa na Tigo kwa kushirikiana na Nlab.

                                                 …………………………………………..

Na Mwandishi Wetu.

 Ijumaa , Novemba 25 , 2022 , Viongozi mbalimbali kutoka Kampuni ya Tigo akiwemo Afisa Mtendaji Mkuu Bwn. Kamal Okba , wameitembelea Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa Iliyoko Ilala Jijini Dar Es Salaam ambayo kwa sasa ni mnufaika wa  mradi wa Tigo e-School unaotekelezwa na Tigo kwa kushirikiana na Nlab , kwa ajili ya kujionea jinsi gani walimu na wanafunzi watakavyonufaika na mradi huo.

Ikumbukwe kuwa mradi huu wa Tigo eSchools umeweza kuunganisha shule mbalimbali na Intaneti ya  4G+ , pamoja na kuweka mfumo wa maudhui kwa ajili ya Wanafunzi kupitia tovuti ya www.tigoeschools.co.tz na kutoa mafunzo ya matumizi ya TEHAMA kwa walimu ili kurahisisha ufundishaji.

Akizungumza katika tukio hilo Meneja Uwajibikaji kwa jamii kutoka Tigo Bi. Rukia Mtingwa amesema kuwa wamefanya hayo katika kutimiza kauli mbiu ya Tigo kuhakikisha kwamba kila Mtanzania anafurahia na kuyaishi maisha ya Kidigitali na pia adhima ya serikali ya kukuza TEHAMA katika shule za Msingi na Sekondari nchini na bado tuna nia na shauku kubwa la kuendelea kutoa huduma hii kwa shule nyingine zaidi nchini. Alimalizia

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa Bwn. Deo Joseph ameipongeza kampuni ya Tigo kwanza kwa kufanya ziara shuleni hapo lakini pia kwa kutekeleza mradi huu wa Tigo eSchools shuleni hapo maana unaenda kubadilisha mazingira ya utoaji na upokeaji wa elimu kwa walimu na wanafunzi shuleni hapo , suala litakalochangia kukua kwa matumizi ya TEHAMA utakaowawezesha wanafunzi kuendana na ulimwengu wa sasa.

” Tunawashukuru sana kampuni ya Tigo kwanza kwa msaada wao kwa kompyuta 10 ambazo wameshatuletea shuleni hapa , lakini pia kwa huduma ya Intaneti ambayo wanatupa kila mwezi kwakweli tunawashukuru na kuwapongeza sana , ila tumewapa ombi jingine la kutuboreshea ” Computer Lab ” yetu ili iwe ya viwango zaidi , tutashukuru sana kama watatutekelezea na hilo ” alimalizia Bwn. Deo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!