Na Shomari Binda-Musoma
MRADI wa maji ya bomba kutoka ziwa victoria uliopo Kata ya Tegeruka jimbo la Musoma vijijini umeendelea kushika kasi kuweza kuukamilisha.
Kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kuweza kuwapatia huduma ya majivictoria. salama wananchi wa Kata huyo.
Katika taarifa iliyotolewa leo septemba 28 na mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema mradi huo unaendelea vizuri na kasi yake inalidhisha.
Amesema Kata ya Tegeruka yenye vijiji vitatu vya Kataryo, Mayani na Tegeruka itatumia maji ya bomba kutoka kwenye Bomba kuu la Mugango-Kiabakari-Butiama lilojengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 70.5
Muhongo amesema chanzo cha maji ya bomba hilo kipo Kijiji cha Kwibara Kata ya Mugango na mitambo iliyojengwa kwenye chanzo hicho ina uwezo wa kuzalisha maji ya ujazo wa lita milioni 35 kwa siku.
Amesema mradi wa zaidi ya shilingi bilioni 4 wa kusambaza maji ndani ya Kata ya Tegeruka umepangwa ukamilike ndani ya miezi miwili ijayo.
“Ujenzi wa Tenki la ujazo wa lita 150,000 unakamilishwa Kijijini Mayani kwa ajili ya usambazaji wa maji ndani ya Kata ya Tegeruka.
“Mabomba ya awali ya kusambazia maji ndani ya vijiji vyote vitatu yameshatandazwa na kasi ya mradi kwa ujumla inaendelea kwa kasi”, amesema Muhongo.
Amesema maji kutoka kwenye bomba hilo yameanza kutumiwa ndani ya Kata ya Mugango yenye vijiji vitatu na Kijiji cha Nyasaungu cha Kata ya Ifulifu nacho kinatumia maji ya bomba hilo
Mbunge Muhongo amedai miundombinu ya usambazaji wa maji ya bomba inajengwa ndani ya Kata za Busambara (vijiji vitatu) na Kiriba (vijiji vitatu) kwa ajili ya kutumia maji kutoka kwenye bomba hilo.
Vijiji vyote 68 vya jimbo la Musoma vijijini vina miradi ya maji ya bomba kutoka Ziwa Victoria na ipo kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji.
Visima virefu vya maji vinachimbwa kwa baadhi ya vijiji vya Kata ya Bugwema ambavyo miradi ya maji kutoka Ziwa Victoria itachelewa kuanza kutekelezwa.
Hadi leo hii, vijiji 54 kati ya vijiji 68 vya kwenye jimbo hill lina asilimia 77.94 ya vijiji vyote vinatumia maji ya bomba yanayotoka ziwa victoria
Viongozi na wananchi wa Musoma vijijini wamemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi kwaajili ya miradi ya maji