BAADA ya Kupikwa kwa miezi nane Vijana wanne wenye vipaji vya Sanaa ya ufundi ngoma,Sanaa za uoni kwa ufadhili wa balozi mbili ikiwemo ubalozi wa Norway na Uswiss wamezitambulisha kazi hizo ramsi.
Akizungumza wakati wa tafrija hiyo Mratibu wa mradi wa “Feel Free” kutoka Taasisi ya Nafasi Arts Space Jijini Dar es salaam, Rhoda Kabenga amesema Balozi hizo mbili zimeweza kuchangia ukuaji mkubwa Sana wa sanaa na Utamaduni nchini Tanzania kwa kuwezesha kutoa Mfuko ambao hauna masharti yoyote na utakaowawezesha wasanii kutengeneza kazi zao za sanaa zenye ubora na viwango.
Aidha Kabenga amefafanua zaidi kuwa ni wito sasa kwa wasanii kuwa wabunifu na kukuza sanaa zao ili waweze kupata wafadhili
na kutangaza kazi zao sambamba na tamaduni zetu na sanaa kwa ujumla.
Nae Mkurugenzi wa Uswazi born Talent (UBT) Meneja Kandoro ambae ni Mnufaika wa Mradi huo kupitia mradi kazi wake wa “Sauti za Kumoyo” ameeleza namna mradi huo ulivyoweza kuwasaidia wasanii wa Muziki wa singeli na kubadilisha taswira kuwa muziki huo sio wa kihuni .
“Mradi huu wa Feel free umeweza kuwaongezea uwezo wa wasanii wa singeli katika namna ya kukuza na kuongeza ufanisi kwenye muziki wao ili kuweza kuongeza mashabiki na kupanua wigo wa wasikilizaji wa muziki wa singeli nje na ndani ya nchi.”
Aidha Kandoro amefunguka zaidi kuwa “sauti za kumoyo” ni mradi ambao umewashirikisha wasanii wa singeli ambapo umechanganywa muziki wa zamani na wa kisasa na kupatikana sauti hizo za kumoyo.
Amewataja wasanii ambao wameshiriki katika Sauti za Kumoyo Kinata Mc,Seneta, Manfongo pamoja na Moto music ambapo Kazi zao wametia vionjo kutoka kwenye makabila tofauti tofauti.