Na Theophilida Felician, Kagera
Wadau mbalimbali wanaohusika na utekelezaji wa programu jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto (MMMAM 2021-2026) wamekutana na kujadili namna ya kuendelea kutekeleza mpango huo kwa ufanisi zaidi ili uweze kuyafikia malengo yaliyokusudiwa.
Mpango huo unaowalenga watoto wenye umri kuanzia mwaka 0-8 umejumuisha maeneo kadhaa ambayo ni ulinzi na usalama wa mtoto, elimu na lishe bora umekuwa ukitekelezwa nchini ikiwemo Kagera kupitia wadau na idara za Serikali zinazohusika moja kwa moja kupitia vitengo vyao pamoja na mashirika ya siyo kuwa ya kiserikali yanayounga mkono bega kwa bega mpango huo.
Mengi juu ya mpango huo yameelezwa kwenye kikao cha wadau kupitia utekelezaji wa majukumu ya mpango huo kwa robo ya Oktoba hadi Desemba 2023 kilichofanyika Manispaa ya Bukoba kilijadili jinsi ya kutilia maanani programu hiyo ambapo zimewasilishwa taarifa kutoka kila halmashauri na wadau.
Taarifa zilizowasilishwa kutoka kila halmashuri zimeambatana na mafanikio yaliyofikiwa pamoja na changamoto.
Taarifa hizo zimeonyesha jinsi kazi inavyofanyika huko kwenye jamii hususani katika utoani wa elimu ya uelewa wa mpango mzima.
Halmashauri ya Missenyi ikiwasilisha taarifa na Afisa ustawi wa jamii Evance Mvungi imefafanua kuwa katika kipindi hicho wametoa elimu kwa njia ya vyombo vya habari, viongozi wa dini, madiwani, walimu wa malezi ya awali 117 wamefikia nakupatiwa elimu nawengine wengi.
Mvungi pia amebainisha kuwa Missenyi imefanikiwa kuwasajili watoto wa chini ya miaka mitano na kuwapa vyeti vya kuzaliwa na jumla ya watoto (31300) wamepatiwa vyeti hivyo sambamba na watoto walio wengi shuleni wanapata chakula.
Amesisitiza kuwa juhudi za kampeni yakuwafikia wananchi na makundi mengine bado zinaendelea kwa kiwango chake.
Afisa ustawi wa jamii Halmashauri ya Bukoba Joyce V. ameeleza kwamba wameyafikia makundi tofauti tofauti na makundi hayo ni wahudumu wa afya ngazi ya jamii 188 walifikiwa, walimu wa mafunzo ya awali, kupima watoto changamoto za ukuwaji watoto 44825 walipimwa ambapo ukondefu walipimwa watoto 456 sawa na 1% na udumavu watoto 235 sawa na 0.5% na katika vipimo hivyo hawakubainika watoto wenye utapiamlo mkali.
Joyce amesema kuwa wao wameenda mbali zaidi katika kumlinda mtoto kwakushirikiana na sekta zote kuanzia elimu, usalama, afya na nyinginezo.
Ameongeza kuwa wamekuwa wakiwafikia hata watoto walio magerezani inapotokea mama zao wamefungwa wakiwa na watoto walio chini ya miaka hiyo 8.
Ametolea mfano wa gereza ambalo wamewahi kufika ni pamoja na gereza la Bukoba.
Taarifa kutoka Halmashauri karibu zote zimeitaja changamoto ya ufinyu wa bajeti ya fedha katika kitengo hicho imekuwa ni moja ya changamoto inayopelekea kutokufanya vizuri kwabaadhi ya majukumu ya utekelezaji wa mpango huo, mfano kutokukaa vikao, mikutano jambo ambalo limejitokeza zaidi katika taarifa ya halmashauri ya Muleba yakutokufanikiwa vizuri kwa robo hii kutokana na changamoto hiyo ya bajeti.
Baada ya suala hilo kuonekana ni shida kidogo Afisa lishe Mkoa Joanitha Jovin amelitolea ufafanuzi akihimiza kila halmashuri ijimudu kulitatua hilo ili majukumu yaende vizuri.
“Suala la hii programu, kuna kitu kipya kimeletwa kuuhusu hii programu? hakuna kitu kipya ni programu jumuishi ilikuwa Afisa lishe anafanya, maendeleo ya jamii anafanya, ustawi anafanya sasa tumeunganishwa pamoja kwamba tunapomuhudumia huyu mtoto twende pamoja katika maeneo matano sasa hapa mtu anaposema tunashindwa kukaa vikao vyakuongelea mlifanya nini kisa hamkuwa na bajeti, ni vikao vingapi vinakaa ndani ya halmashauri? tumieni kolamu ya vikao vyenu kwa sababu tuliwahesabia wale watu watano kila vikao vya kila halmashauri wamo vikao vyakamati ya lishe wale wote wajumbe watano niwajumbe wakamati yalishe kwa maelekezo ya Mhe RC Afisa ustawi wa jamii aingie kwenye kamati yalishe, kwakufanya hiyo tutaona niwapi tumepungukiwa tunatoka wapi tunaenda wapi, kwahiyo kusema kukosa kufanya kama halmashauri ya Muleba ilivyowasilisha hapa kila kitu hakijafanyika!kila kitu hakijafanyika! nikosa kutwambia kwamba hakikufanyika kwa ajili ya bajeti, wakuu wawilaya walielewa, wakurugenzi wakaelewa na Kagera ni Mkoa tulifanya vizuri kwahiyo hilo la bajeti tulitowe kichwani” amefafanua Afisa lishe Joanitha.
” Hata hivyo kwenye vikao vya halmashauri ambavyo havijatengewa bajeti hata Mkoa huwa hatufanyi vikao hivyo? tunafanya watumishi wa serikali ni mara ngapi tunajikopesha kwahiyo tunaposema kiulahisi hatujafanya kitu kwa sababu ya ufinyu wa bajeti siyo nzuri, ripoti hii ikipelekwa kwa viongozi utakuwa na barua yakujibu tumelewana wenzangu? tusichukulie vitu kilahisi lahisi” mpaka serikali tuiwekee mrorongo miiongozo ije manake ina hitaji tuifanyie kazi, kwahiyo tusisingizie bajeti kutokufanya kazi zilizoko mbele yetu”.ameendelea kutoa maelezo Afisa Joanitha mbele ya wadau.
Kwa pande wake Abemelek Richard kutoka shirika la TADEPA wanaohusika kwa njia mbalimbali katika kutekeleza mpango huo na wajumbe wengine wameshauri kuwa taarifa zinazoandaliwa na kuletwa kwenye vikao ziwe zenye kuonyesha uhalisia kwakina hali ya mambo yalivyo huko kwenye jamii kuanzia shuleni, majumbani na kwingineko maana hiyo itasaidia kufahamu mpango huo unatekelezwa kwakiwango gani na mafanikio yapi.
Kwa pamoja wadau walioshiriki kikao hicho akiwemo Afisa maendeleo ya jamii Mkoa Issa Mrimi, Martin Rwabilimbo kwaniaba ya mganga Mkuu wa Mkoa maafisa ustawi, lishe, elimu, maendeleo, mashirika wote wameazimia kuendeleza mapambano kwakila namna ili mpango huo uwe wenye matunda kwa watoto lengwa kwani bado changamoto zinazowakabili ni nyingi kupitia maeneo tofauti tofauti hususani ya ukatili.