Na Shomari Binda-Musoma
HALMASHAURI ya manispaa ya Musoma imepokea na kuzindua mpango jumuishi wa taifa wa malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto( PJT-MMMAM) wa mwaka 2021/2023 na 2025/2026.
Akizindua mpango huo kwenye kikao cha jukwaa la uwezwshaji wanawake kiuchumi manispaa ya Musoma,Naibu Meya wa manispaa hiyi Naima Minga amesema mpango huo ni mzuri na wapo tayari kuutekeleza.
Amesema mtoto anapaswa kuwa na makuzi bora pamoja na malezi na kupelekea serikali kuja na mpango huo jumuishi.
Naibu Meya huyo amesema wanawake wanao wajibu mkubwa wa kumuangalia mtoto na kwa kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali watahakikisha wanautekeleza kama ilivyo kusudiwa.
“Mpango huu ni mzuri na tumeupokea na kuuzindua kwaajili ya utekelezaji wake kwenye halmashauri yetu ili kufikia malengo kusudiwa.
“Serikali inayo nia njema na watoto wetu na kuja na mpango huu na sisi kama tulivyouzindua tupo tayari kutekeleza kwenye maeneo yetu”,amesema Naima.
Amesema licha ya kuangalia makuzi ya mtoto anapswa pia kukingwa na kumuepusha na kujiingiza kwenye matendo yasiyofaa yakiwemo ya nshoga na kusagana.
Aidha amewataka wanawake kutumia vizuri fedha za mikopo wanayoipata kwenye halmashauri kuendeleza biashara na kirejesha ili kuweza kimuhudumia mtoto na kurejesha
Mkuu wa kitengo cha mipango,uchumi na maendeleo kutoka Kanisa la AICT-Tanzania Charles Mashauri wanaosimamia mpango huo ameipongeza halmashauri ya manispaa ya Musoma kwa kuzindua mpango huo.
Amesema kwa maelekezo ya mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda baada ya kuzindua kimkoa maelekezo yalitolewa kwa halmashauri zote kukamilisha uzinduzi kabla ya mwezi novemba kumalizika.
Amesema dhamira ya serikali kuwekeza katika mpango wa makuzi,malezi na maendeleo ya awali ya mtoto ni kulenga kwenye lishe pamoja na afya bora.
Mashauri amesema mpango huo wa MMMAM unaangalia pia ulinzi na usalama wa mtoto ikiwa ni pamoja na kuzuia vitendo vya ukatili wa. kijinsia,ajali,unyanyasaji wa kihisia,kimwili na ngono.