Home Kitaifa MP KILANGO: RAIS SAMIA AMEFANYA MAMBO MAKUBWA SAME

MP KILANGO: RAIS SAMIA AMEFANYA MAMBO MAKUBWA SAME

Ashrack Miraji, Same Kilimanjaro

Mbunge wa jimbo la Same Mashariki, Anne Kilango amesema hayo leo Machi 19 2024 wakati wa uwasilishaji wa mafanikio ya miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita Chini ya Uongozi Mahiri wa Dkt. Samia Suluhu Hassan huku akijivunia mafanikio makubwa kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali katika Jimbo lake.

Mhe. Kilango alisema chini ya uongozi mahiri wa raisi Dkt. Samia Suluhu Hassan wananchi wengi wamesikika na wamefikiwa kwa kuboreshewa na kutatuliwa kero na matatizo yao yaliyokuwa yanawasumbua ikiwemo maji, barabara, umeme, afya na miradi ya boost.

“Kiukweli nipende kutoa shukran zangu za dhati Kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na kumpongeza kwa miaka yake mitatu amefanya mabadiliko makubwa katika sekta ya uchumi kwenye Taifa letu hasa Kwa wananchi wangu wa Jimbo la Same mashariki” amesema na kuongeza;

“Baadhi ya mafanikio hayo ni pamoja na kuunganisha umeme vijijini (REA), kujenga vituo vya Afya na madarasa katika tarafa tofauti na Kata zake kupita mradi wa boost katika Jimbo Same Mashariki, kutujengea barabara ya Hedaru, Vunta ma Mambamiamba chini ya wakala wa barabara vijijini TARURA”.

Aidha, Kilango ametoa rai kwa wananchi wa Jimbo lake na taifa kwa ujumla waendelee kumuunga mkono Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya katika Taifa la Tanzania na ujasiri anaowapa hasa katika kulipigania Taifa letu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!