Home Michezo MO AAHIDI KUFANYA USAJILI BORA KWA KLABU YA SIMBA

MO AAHIDI KUFANYA USAJILI BORA KWA KLABU YA SIMBA

Muwekezaji wa Klabu ya Simba Mohamed Dewji (Mo) amewaahidi Mashabiki wa Simba na wapenda soka kiujumla kuboresha Klabu hiyo kwa kusuka upya benchi la ufundi na kufanya usajili bora.

Tumeshindwa kutengeneza timu bora ya ushindani eneo la benchi la ufundi halikuwa zuri hali ambayo imepelekea kupotea hata kwa falsafa yetu ya mpira biriani, hili ni eneo la kufanyia kazi naahidi tutashirikiana na viongozi wenzangu kusuka upya benchi la ufundi, la tatu tumeshindwa pia kukidhi kiu ya Wanasimba katika usajili wachezaji wengi ambao wamesajiliwa viwango vyao havikuwa bora, kwahiyo ningependa kuahidi Wanasimba nitashirikiana na viongozi wenzangu na wataalamu kufanya usajili bora na katika ukubwa utakao kidhi matamanio ya Wanasimba” amesema Mo

Amesema hayo 12 June 2024 kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram wakati akitoa tathmini ya Klabu hiyo kwa misimu kadhaa iliyopita ambayo imepoteza takribani vikombe vyote vikubwa vya ndani kwa misimu mitatu mfululizo pamoja na kuishia robo fainali katika michuano ya bara la Afrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!