Na Magrethy Katengu
Wadau, Kampuni, Taasisi za serikali na zisizo za kiserikali, Mashirika na Mtu binafsi wameshauriwa kuwa na moyo wa kutoa sehemu ya hali na mali kusaidia kwa kurudisha kwa jamii kwa kusaidia ikiwemo hospitali kwa wagonjwa kwani kutoa ni moyo wala si utajiri na Mungu hupenda moyo mkarimu.

Ushauri huo umetolewa Jijini Dar es salaam na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo wakati akikabidhiwa msaada wa vifaa vya hospitali na Lion Clubs International shirika linaloongoza kwa kutoa huduma duniani kusaidia jamii ambambo amesema vitu wanavyovipokea vinakwenda kuongeza kasi zaidi katika vituo vya afya katika wilaya hiyo
“Tunashukuru kwa mioyo yenu mikunjufu Mungu aliyowapatia imeamua kuja katika wilaya ya Korogwe kugusa jamii kwani naamini mnatambua papote kwenye jamii kuna changamoto hivyo mmeonyesha moyo na mmeinyesha njia wengine kuiga mfano huu” amesema Mkuu wa Wilaya

Naye Mwakilishi wa Lion clabu Bhavika Sajan Licha ya kua tunatoa huduma katika njia nyingi juhudi zetu tumezikita katika maeneo makuu matano ili kuigusa zaidi jamii. Maeneo haya matano ni miongoni mwa mambo muhimu na yanayosumbua ulimwengu kwa kiasi kikubwa dira na yetu ni kurudisha kwa jamii inayotuzunguka,huduma zetu zimejikita katika maeneo kama vile Mazingira, Kupambana na njaa, Kisukari, Macho pamoja na Saratani kwa Watoto..
“Tunasema kua kila kwenye uhitaji basi Lions tupo na Kadri tunavyokua pamoja ndivyo tunavyotoa huduma nyingi zaidi. Mchango wetu ni Jenereta ya 2KVA, Viti sita vya Magurudumu na Mashine sita za kidijitali za kupima Presha tunatarajia kuendelea kushirikiana zaidi na Wodi hii ya watoto katika siku zijazo” amesema Sajan
Aidha Lions Clubs International imegawanyika katika maeneo kadhaa duniani huku ikiwa na wanachama wapatao Milioni Moja nukta nne (1.4). Kwa Afrika,Tanzania ipo katika ukanda wa 411 ikiwa ni sehemu ya kanda jumuishi ambapo inahusisha nchi jirani kama Kenya,Uganda,Ethiopia na Visiwa vya Shelisheli. Tanzania inafahamika kama kanda 411 C ikiwa na klabu takribani Ishirini na Nne na wanachama Mia Sita Ishirini mpaka sasa.
Kazi za Lions zinaanzia kwenye jamii na kila jamii ina mahitaji yake muhimu.
