![](https://www.mzawa.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250211-WA0157-1024x682.webp)
Mkuu wa Shule ya Sekondari Sumve amepongeza mafanikio yaliyopatikana ndani ya kipindi cha utawala wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza jana, Mkuu wa Shule ya Sekondari Sumve, Bi. Clotilda Elly, alisema kuwa shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani mbalimbali ya kitaifa tangu kuingia madarakani kwa Rais Samia Suluhu Hassan. Hii ni kutokana na juhudi za Serikali zilizotokana na uongozi wake, ambapo fedha nyingi zimetolewa kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule, ikiwemo ujenzi wa mabweni manne yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 80 na matundu 16 ya vyoo.
Bi. Clotilda alisema kuwa, kutokana na kuboresha miundombinu ya shule, wanafunzi katika shule hiyo wameendelea kufanya vizuri, ambapo hadi kidato cha nne, wanafunzi wavulana ni 467 na wasichana 1710, jumla ya wanafunzi 2,177. Aidha, katika shule ya vidayo vya juu, kuna jumla ya wanafunzi 778.
Mkuu huyo wa shule aliongeza kwa kusema kuwa, kazi kubwa zilizofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kuboresha mazingira ya elimu ni za kupigiwa mfano. Aliwaomba Watanzania kuendelea kumwamini Rais Samia ili aweze kufanya makubwa zaidi katika maendeleo ya nchi.