Home Kitaifa MKUTANO WA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI KUFANYIKA DAR ES SALAAM NOVEMBA 19HADI...

MKUTANO WA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI KUFANYIKA DAR ES SALAAM NOVEMBA 19HADI 21

Na Magrethya Katengu —Dar es salaam

Tanzania ni miongoni mwa nchi iliyoweka msingi thabiti wa kushirikiana na wadau mbalimbali katima sekta ya Madini ili kuhakikisha raslimali hiyo inaleta manufaa katika Ukuaji wa Uchumi na kuongeza pato la Taifa.

Ameyasema hayo leo Novemba 14, 2024 Jijini Dar es salaam Waziri wa Madini Anthony Mavunde katima mkutano na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa kuhusu
Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini unatarajiwa kufanyika nchini Tanzania na kuhudhuriwa na washiriki 1500 ndani na nje ya nchi na kuongozwa na kauli mbiu ya mwaka huu, “Uongezaji Thamani Madini kwa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii”, itasisitiza umuhimu wa kuongeza thamani ya madini ili kuleta faida zaidi kwa taifa

Mkutano huo utakuwa na mada mbalimbali na watoa mada zaidi ya 50 kutoka ndani na nje ya nchi, wakiwemo mawaziri wa madini kutoka nchi za Afrika, wawakilishi wa kampuni kubwa za madini duniani, na mabalozi wa nchi 31.

“Mkutano huu utatoa fursa ya kujifunza kuhusu sera, mikakati mipya ya serikali, na kujadili masuala ya kisheria na kiuchumi yatakayohusiana na madini hivyo huu ni wakati muafaka kwa wawekezaji na wafanyabiashara kujifunza kuhusu fursa zinazoendelea kutokea nchini Tanzania, hususan katika viwanda vya uchakataji madini” amesisitiza Waziri

Waziri Mavunde amesema Sekta ya madini inachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa Tanzania. Katika Mwaka wa Fedha 2022/23, sekta hiyo ilichangia zaidi ya asilimia 56 ya mapato ya kigeni kupitia mauzo ya bidhaa za madini nje ya nchi, na asilimia 15 ya kodi za ndani zinazotokana na shughuli za madini. Pamoja na mchango huo mkubwa, Serikali ya Tanzania inataka sekta ya madini ichangie asilimia 10 ya Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025.

Aidha Mkutano huo ni wasita (6), utakaofanyika kuanzia tarehe 19 hadi 21 Novemba 2024 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC),ambapo Utafunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ukienga kuendeleza sekta hiyo inayokua kwa kasi, huku ukileta manufaa ya kiuchumi na kijamii kwa Watanzania na dunia kwa ujumla.

Pia kutakuwa na hafla ya “Usiku wa Madini” tarehe 20 Novemba, 2024, ambapo tuzo zitatolewa kwa wadau waliofanya vizuri katika sekta ya madini. Hafla hii pia itakuwa na maonesho ya bidhaa za madini, ikiwa ni pamoja na vito vya thamani na madini ya viwandani, ili kuonyesha fursa zilizopo na umuhimu wa madini katika maisha ya kila siku ya Watanzania.

Mkutano huo utahitimishwa siku ya tarehe 21 Novemba 2024 na Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!