Home Kitaifa MKUTANO WA HADHARA MKOA WA DAR ES SAALAM WANANCHI WAJIONEA WANAYOTENDEWA NA...

MKUTANO WA HADHARA MKOA WA DAR ES SAALAM WANANCHI WAJIONEA WANAYOTENDEWA NA SERIKALI YAO KUPITIA ILANI YA CCM

Na Magrethy Katengu

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es salaam Abbas Mtevu ametoa wito kwa wananchi wote kuachana kabisa na maneno ya wanaozungukazunguka kuwalaghai ili wasiwe na Imani na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa yale yote anayoyatekeleza kupitia ilani ya CCM 2020-2025 kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo katika sekta ya Elimu,Afya, uchukuzi na ujenzi.

Ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam Jimbo la Ilala uliofanyika Kariakoo katika Mkutano wa hadhara wa wananchi uliojumuisha kata zote 4 na viongozi wote wa CM kuanzia ngazi ya Wilaya kata na kijiji na katika mkutano huo wenyeviti wa serikali za mitaa vitongoji na makatibu wao wamepatiwa vyeti vya kutambua mchango wao wa kusaidia serikali katika ukamimilikaji wa maradi katika kata zao ikiwemo ujenzi wa Madarasa ya Shule ya msingi, zahanati na barabara

“Ninashangazwa sana na hao wanao wanaozunguka huko na huko kumtukana Rais kusema hafai na anauza Bandari wakati Miaka ya nyuma walizuiwa kufanya mikutano ya hadhara na walikaa kimya wengine walikimbia nchini na kwenda nje ya nchi lakini Rais Dkt Samia kwa upendo na ukomavu wake wa kisiasa akawafuata huko walipo na kuwaambia warudi atahakikisha atawalinda na kuwaruhusu kufanya mikutano ya hadhara lakini cha kushangaza hao hao ndiyo wamemgeuka na kumdhihaki watanzania nawasihi fanyeni shughuli zenu za kiuchumi wapuuzeni” amesema Mtemvu

“Serikali iliyoko madarakani unawapenda wananchi wake na imekuwa ikifanya jitihada kuwakwamua na umasikini na imetoa pesa kuwasadia jukumu la kuwatatulia Wananchi changamoto zao kupitia mikopo ya asilia 10 inayotolewa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kuwapatia uhuru sasa wamemgeuka msiwasikileze” amesema Abbasi

Nae Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa CCM Juma Simba Gadafi amesema baadhi ya Wananchi wanakibeza Chama hivyo wanahakikisha wanaleta maendeleo mbalimbali Nchini bila kujali Dini, kabila wala Chama.

Sambamba na hayo pia Gadafi amewataka Wananchi kumuunga Mkono Mbunge wa Jimbo hilo ambae pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Azan Zungu amenshukuru Mbunge huyo kwa kutafuta miradi mbalimbali kuhakikisha changamoto mbali zinazo wakabili Wananchi wa Ilala kupitia ilani ya CCM zinapatiwa ufumbuzi ikiwemo kujenga matundu ya vyoo, kujenga barabara.

Naye Naibu spika ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilala Hassan Zungu amewataka wananchi wa Jimbo hilo kuwa na Imani na Chama cha Mapinduzi wasipotoshwe na maneno wasiokuwa hata na aibu kumtukana Rais bila kuangalia wapi alipowatoa kisiasa akawaita ikulu kuzungumza nao juu ya maridhiano ya kisiasa

Aidha siku hiyo ilikuwa ya kipekee sana kwani kulikuwa na zoezi la ugawaji kadi miatisa themanini kwa wanachama wapya na Ugawaji vyeti vya pongezi kwa Wenyeviti wa serikali za mitaa pamoja na makatibu wake

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!