Na Scolastica Msewa, Kibaha.
Chuo kikuu Cha nchini Marekani kimemtunukia Udaktari wa heshima Mkurugenzi (PhD) Mtendaji Jukwaa la Wazalendo huru Dk. Mohamed Mwampogwa kwa utumishi uliotukuka anaofanya kwa jamii na Chuo Kikuu cha All Nations Christian Church International University kilichopo Texas Marekani (ANCCI) kutokana na mchango wake kwenye jamii.
Sherehe ya kutoa shahada hiyo kwa watu mbalimbali imefanyika leo Kibaha kwa Mbonde Mkoa wa Pwani ambapo Mwakilishi wa chuo hicho ambaye ni raia wa Kenya, Profesa Purity Gatobu alitunuku Shahada hiyo.
Akizungumza mara baada ya kutunukiwa Shahada hiyo, Dk. Mwampongwa ameshukuru kwa Chuo kikuu hicho kutambua mchango wake kwa jamii hata kumtunukia Udaktari huo wa heshima.
Dkt. Mwampongwa amesema Shahada aliyotunukiwa imempa ari ya kuendelea kutumikia jamii kwa kutoa msaada mbalimbali kwenye jamii.
Aidha amepongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha utaratibu wa kusikiliza kero za Wananchi na amewataka viongozi wa Chama na serikali kutimiza wajibu wao kwa kushughulikia kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili Wananchi
Naye Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa la Wazalendo huru taifa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo mkoa wa Pwani Hadija Juma amesema Kila kiongozi katika nafasi yake atatue changamoto na kero za Wananchi ili kumrahisishia kazi Mheshimiwa Rais.
Hadija amesema jukwaa hilo litaendelea kuhudumia Wananchi kwa kushiriki shughuli mbalimbali za Maendeleo katika jamii.
+++++++++++