Home Kitaifa MKURUGENZI SINGIDA APEWA SIKU 5 KULIPA DENI LA TSH MILIONI 29.2

MKURUGENZI SINGIDA APEWA SIKU 5 KULIPA DENI LA TSH MILIONI 29.2

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi wa Singida Mjini ya kumtaka kulipa deni la Tsh Milioni 29.2 ndani ya Siku 5 hadi kufikia tarehe 30 Januari mwaka huu.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya Mwl. Allan Climent ambaye alishastafu tangu mwaka 2021 kumueleza Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda ya kudai mafao yake bila mafanikio yoyote na kueleza zaidi ya kwamba yeye ni mgonjwa wa moyo.

Naye, Mwenezi Makonda amesema “haiwezekani Mtu anadai stahiki zake tangu mwaka 2021 tena ni mgonjwa lakini hapati haki yake, huo sio utaratibu wa Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia huo ni uzembe wenu tu kazini..mbona mishahara yenu hamsubirii mpaka miaka 5 ndio mlipwe? Natoa siku 5 kama maelekezo ya CCM Mwalimu huyu mstaafu alipwe pesa zake”

Makonda ametatua kero hiyo wakati akizungumza na Wananchi wa Singida kwenya Mkutano wa Hadhara uliofanyika leo tarehe 25 Januari, 2024 ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya Mikoa 20 Back To Back.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!