Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, Karia Magaro, ameongoza timu ya menejimenti kukagua miradi ya maendeleo katika kata za Nyamigota, Ludete, na Katoro.
Ziara hiyo ilihusisha ukaguzi wa miradi mikubwa ya ujenzi yenye thamani ya mabilioni ya shilingi, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha utekelezaji wa miradi unafanyika kwa ufanisi na kwa wakati.

Miradi Iliyotembelewa na timu hiyo ni pamoja na mradi wa
1. Shule ya Amali Chibingo – Thamani: TZS milioni 584.28.
2. Upanuzi wa Miundombinu ya Kidato cha 5 na 6:
Sekondari ya Kagega (TZS milioni 481).
Sekondari ya Lutozo (TZS milioni 381).
3. Shule ya Msingi Afya – Madarasa 9 yaliyojengwa kwa TZS milioni 351.5 kupitia Mfuko wa BOOST.
4. Shule ya Sekondari Katoro – Miradi katika hatua za awali, thamani TZS milioni 584.28.
Ambapo Menejimenti ilibaini ucheleweshaji wa vifaa vya ujenzi, unaosababishwa na wazabuni kushinda zabuni nyingi zaidi ya uwezo wao.
Mafundi wamekuwa wakikaa muda mrefu uwandani bila vifaa vya ujenzi, hali inayochelewesha ukamilikaji wa miradi.
Kamati za usimamizi wa miradi zinalazimika kusimama kazi kwa kukosa vifaa muhimu.
Mkurugenzi Magaro alionyesha kutoridhishwa na hali hiyo na kutoa maagizo kwa wazabuni kuhakikisha vifaa vinafika kwa wakati, vinginevyo mikataba yao itaenguliwa.
Mkurugenzi Magaro alitoa pongezi kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi kwa miradi ya maendeleo, akisisitiza kuwa Serikali ya Wilaya itaendelea kusimamia rasilimali hizi kwa manufaa ya wananchi.
Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Geita imesisitiza dhamira yake ya kuhakikisha miradi yote ya maendeleo inakamilika kwa wakati, ikiwemo kuimarisha miundombinu ya elimu ili kuleta maendeleo ya haraka kwa wananchi.
Mwisho..