Home Kitaifa (MKUMBI) UMEFANIKIWA UFUTAJI NA UPUNGUZAJI WA TOZO, ADA NA FAINI 232

(MKUMBI) UMEFANIKIWA UFUTAJI NA UPUNGUZAJI WA TOZO, ADA NA FAINI 232

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amesema Utekelezaji wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (MKUMBI) umefanikiwa ufutaji na upunguzaji wa tozo, ada na faini 232 na kupitia na kurekebisha Sheria 40 zilizokuwa zinaleta changamoto katika ufanyaji biashara na uwekezaji nchini.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo wakati akifungua Semina ya Wahariri wa Vyombo vya Habari, Waandishi wa Habari pamoja na Watengeneza Vipindi vya uwekezaji, viwanda na biashara iliyolenga kutoa elimu kuhusu Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini ( MKUMBI) iliuofanyika Novemba 7, 2022 JNICC Dar es Salaam.

Aidha amesema utekelezajibwa MKUMBI pia umefanikiwa kuondoa urudufu wa majukumu na kuunganisha taasisi zenye majukumu yanayoingiliana kama TBS na TMDA, kuanzisha mifumo ya Tehama,
kuimarisha vituo vya utoaji huduma za mahali pamoja kama TIC na kuanzishawa dirisha moja la kielektroniki la utoaji huduma kwa wawekezaji.

Akiongea na washiriki hao, Dkt. Kijaji ameelezea misingi 10 inayopaswa kuzingatiwa katika utekelezaji wa MKUMBI inayolenga kuboresha utendaji kazi na utoaji huduma kwa umma kwa uwazi, kufanya maamuzi kwa mujibu wa sheria na kuongeza uwajibikaji katika sekta ya umma pamoja na kuimarisha majadiliano na ushirikishaji wa sekta binafsi.

Ametaja misingi hiyo kuwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa Maboresho yanayofanywa na mamlaka za udhibiti yasilenge kuongeza mapato bali kukidhi gharama za utoaji huduma, Ukusanyaji wa mapato utumie nyezo rahisi na rafiki kwa kuweka vituo vya pamoja vya huduma au kuunganisha mifumo na Kuondoa mwingiliano wa majukumu ya taasisi na kuunganisha majukumu yanayofanana .

Misinging mingine ni kuhakikisha Sheria, Kanuni na Taratibu zinatekeleza sera ya biashara, ushindani, kumlinda mlaji na huduma za umma; Udhibiti uwe kwa lengo la kuendeleza sekta husika au uzalishaji; Kukuza ushindani wa kimkakati wenye usawa, tija na ubunifu, kwa kupunguza tozo na ada; Kuwa na mifumo ya udhibiti yenye uhakika, endelevu na inayotabirika; Kanuni zote zitakazotungwa zifanyiwe tathmini ya athari ya udhibiti kabla ya kuidhinishwa kutumika; Kuhakikisha kuwa maboresho ya kupunguza kanuni hayaondoi mamlaka ya Mamlaka za Udhibiti; na Kutatua chagamoto za kiutendaji ndani na baina ya Mamlaka za Udhibiti. Amesema Dkt. Kijaji

Aidha, Katika kuhakikisha kuwa mpango wa kuboresha biashara na uwekezaji unatekelezwa kwa ufanisi, Waziri Kijaji amesema Serikali pia imefanikiwa kuanzisha Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, kwenye mamlaka zote za Serikali za Mitaa ambazo zimeanza kutekeleza majukumu yake tangu tarehe 1/7/2022.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bw. Ally Gugu, amesema Semina hiyo imelenga kuwaelimisha wahariri na waandishi wa habari za biashara kuelimisha umma hususani jumuiya ya wafanyabishara na wawekezaji waweze kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza kulingana na maboresho hayo pamoja na kusisitiza Taasisi zinazotoa huduma kwa wafanyabiashara ziendelee kutoa huduma hizo kwa wakati, ufanisi na tija zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!