Theophilida Felician Kagera.
Jamii ya mwambao wa Tarafa ya Bugabo Halmashauri ya Bukoba mkoani Kagera imehimizwa kujimudu na kutilia mkazo wa kuwapatia elimu stahiki watoto wao.
Wito huo umetolewa naye Mkufunzi wa chuo cha ualimu Katoke kilichopo wilaya ya Muleba Mkoani Kagera mwalimu Hans Arnold Bigilwa akiwa Mgeni rasmi katika Mahafali ya kumaliza darasa la saba mwaka 2023 shule ya msingi Ikondo iliyopo kitongoji cha Nyakaralo Kijiji cha Kyamarange Kata ya Rubafu Halmashauri hiyo ya Bukoba.
Mkufunzi Hans Ameeleza kwamba jamii ya ukanda huo kwa sasa imekuwa haina mwamko thabiti juu ya suala zima la elimu kama ilivyo kuwa miaka ya nyuma hali ambayo imepelekea kiwango cha wasomi kutokea ukanda huo kushuka ukilinganisha na vipindi vya miaka ya nyuma.
“Kimsingi sisi tunaludi nyuma badala yakusonga mbele hapa katikati tunapotea ndugu zangu tunahitaji kufanya kitu Bugabo kitaaluma, mimi ni mwalimu tena bahati nzuri mwalimu wa walimu kutokea chuo cha Katoke tunaposajili mwaka wakwanza huwa naangalia Bugabo wamekuja wangapi? kuna miaka tunapita hivi hivi bila ya mtu hata mmoja nikwasababu tumeacha kushughulika na elimu” ameeleza mbele ya wazazi na wanafunzi Mkufunzi Hans.
“Inaonekana sisi suala la elimu bado tunachangamoto nalo tunaendelea kutegemea ambao walisoma lakini tunasahau kwamba binadamu muda wetu wakuishi ni mchache nakuishi kwetu ni mzunguko sisi tunaisha tunatoka wengine wanakuja ambao ni hawa sasa msipowapa msisitizo hawa ili waingie kwenye nafasi zetu mtajikuta mnasombwa ndo hapo tutakaribisha tena ukoroni tukikosa wasomi tukakosa watu tuliowatengeneza akili mwisho wasiku hapa utanunuliwa naukinunuliwa wewe unakuwa mpagasi kwenye shamba lako kwa hiyo niwaombe ndugu zanguni wa Ikondo tufanyie bidii elimu Bugabo tunaendelea kuchekwa kwa sasa hivi” ameendelea kusema bayana Hans Arnold.
Katika msistizo huo wa elimu amewasihi wazazi nawalezi kujitahidi kushiriki kuchangia michango inayohitajika shuleni pale Serikali inapokuwa haijafika kutimiza hilo hususani suala la ujenzi wa mabweni kwa shule ya Sekondari Katale ambapo ametolea mfano wajitihada wanazozifanya wananchi wa wilaya ya Karagwe katika kuchangia suala la ujenzi wa mabweni na imepiga hatua kwakiwango kikubwa katika hilo.
Hata hivyo amepongeza juhudi zinazofanywa na walimu washule hiyo nakupelekea watoto wanaosomea shuleni hapo kufaulu vizuri katika mitihani ya kitaifa kwa madarasa ya nne na saba, hivyo amechangia mifuko minne ya Saruji kuunga juhudi za utatuzi wa changamoto zinazoikabili shule hiyo ya Ikondo.
Viongozi na watendaji kutoka kata hiyo ya Rubafu wamejitokeza nakushiriki mahafali hayo ambapo Afisa Elimu kata Eustadi Katunzi pamoja naye Afisa mtendaji wa kata Projestus Mwombeki nao wamezidi kutoa maelezo ya kuwahimiza wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanatimiza wajibu wakuwatimizia mahitaji watoto wakiwemo waliomaliza darasa la saba na kwawale ambao bado wanaendelea na safari ya masomo.
Kwa upande wake mwalimu Mkuu wa shule hiyo akisoma taarifa ya shule Rangton Byarugaba Ijumba amesema kuwa shule hiyo ilianzishwa mnamo Tarehe 1 Julai mwaka 1975 ina wanafunzi 351, wapo walimu 4 wakiume na wakike 1 wakuajiriwa pamoja na walimu 2 wakujitolea, yapo madarasa 7 kati 8 yanayohitajika, nyumba za walimu 3 kati ya 5 zinazohitajika, matundu ya vyoo 10 kati ya 16 yanayohitajika.
Sambamba na hayo amebainisha kuwa ufaulu wa wanafunzi kwa darasa la 4 nala 7 kwa kipindi cha miaka minne umekuwa mzuri kwa kila matokeo.
Ameyataja mafanikio kwakipindi cha miaka miwili kuwa wamekarabati shule kutokana na nguvu za wazawa waliosomea shule hiyo, kupata madawati yakisasa 22 pia kujenga choo ya walimu na nyinginezo, huku changamoto zikiwa ni upungufu wa walimu watatu, upungufu wa matundu sita ya vyoo vya wanafunzi naupungufu wa nyumba mbili kwani hata tatu zilizopo zinahitaji ukarabati mkubwa.
Faustin Anjero ni mwenyekiti wa kamati ya shule amewashukuru wadau wote hasahasa wazawa waliokwisha fanikiwa walioko ndani ya nchi na nje ya nchi kwa namna ambavyo wamekuwa wakijitahidi kutatua changamoto zanazoikabili shule hiyo ambayo ina miaka 48 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1975.
Jumla ya wanafunzi 62 wamefanikiwa kumaliza darasa la saba katika shule hiyo.