Home Kitaifa MKALIPA AWATAKA WANAFUNZI KIMANI SEKONDARI KUWA WAZALENDO KWA TAIFA

MKALIPA AWATAKA WANAFUNZI KIMANI SEKONDARI KUWA WAZALENDO KWA TAIFA

Katibu wa UVCCM Wilaya ya Kisarawe ndugu Nasri Mkalipa amewataka wanafunzi Kimani Sekondari kuwa wazalendo pamoja na kutunza tunu ya amani na utulivu ili kuchochea maendeleo kwa Taifa.

Wito huo ameutoa leo Ijumaa 01 Julai, 2022 wakati alipokuwa mgeni rasmi katika sherehe ya kuwakaribisha wanafunzi wa kidato cha tano katika shule hiyo iliyopo Kata ya Kisarawe ambapo aliambatana na Afisa Tarafa wa Tarafa ya Sungwi ndugu Kazimir Kombo.

Vijana tusome kwa bidii Ili tuweze kuzifikia ndoto zetu kwa lengo la kuja kulitumikia Taifa letu Tanzania ,kwahiyo tuendelee kusoma na kufaulu ili tuwe mfano kwa vijana wengine waliopo nyuma yetu alisema Mkalipa.

Katika hatua nyingine ndugu Mkalipa aliwataka vijana kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika tarehe 23 August, 2022.

Tunawajibu wa kuhakikisha watu wengi wanahesabiwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika tarehe 23 Agosti, 2022″ alisema Mkalipa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!