Home Kitaifa MIUNDOMBINU YA KUSAMBAZA UMEME NI YA MUDA MREFU – DKT. BITEKO

MIUNDOMBINU YA KUSAMBAZA UMEME NI YA MUDA MREFU – DKT. BITEKO

📌Asema ilijengwa wakati mahitaji yakiwa kidogo

📌Vijiji vyote vimefikiwa na umeme

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema miundombinu iliyopo ya kusambaza umeme ni ya muda mrefu na Serikali tayari imeshaanza kazi ya kuibadilisha.

Dkt. Biteko ameyasema hayo wakati akiwa katika kipindi cha dakika 45 ITV Januari 20,25.

“Miundombinu hii imekuwepo kwa miaka mingi, ndio maana tumeanza kufanya matengenezo kwa kuondoa ya zamani na kuweka mipya”. Amesema Dkt. Biteko.

Ameongeza kuwa kazi kubwa imefanyika kwenye kusambaza umeme Vijijini ambapo takribani asilimia 100 ya vijiji vyote vimefikiwa na nishati ya umeme.

Adha, utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini hivi sasa unaelekea kwenye Vitongoji ambapo kati ya Vitongoji elfu 64 nchini Vitongoji elfu 34 vimefikiwa na nishati ya umeme.

Dkt. Biteko amesema matumizi ya umeme hivi sasa yameongezeka katika sekta nyingine za kiuchumi ikiwemo treni ya SGR, kwenye migodi mikubwa na midogo ambayo haikuwa imeunganishwa na umeme hivi sasa imefikiwa na nishati hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!