Home Michezo MISRI MWENYEJI WA MASHINDANO YA MICHEZO AFRIKA 2027

MISRI MWENYEJI WA MASHINDANO YA MICHEZO AFRIKA 2027

Tanzania imeungana na baadhi ya nchi wanachama wa Baraza la Michezo la Umoja wa Afrika kuichagua nchi ya Misri kuwa mwenyeji wa Mashindano ya 14 ya michezo ya Afrika ( All African Games 2027).

Tanzania imewewakilishwa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma katika Kikao hicho maaalum cha Kamati ya kiufundi ya nne kuhusu vijana, utamaduni na michezo (STC – YCS- 4) Jijini Accra Ghana Machi 9, 2024.

Kikaoo hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. Uchizi Mkandariwe ambaye ni Waziri wa Vijana na Michezo wa Jamhuri ya Malawi, ambacho kimefanyika Kando ya mashindano ya All African Games yanayoendelea nchini humo ambapo Tanzania inashiriki katika michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu kwa wanawake chini ya miaka 20, kuogelea, baiskeli, judo, ngumi na kriketi.

Mhe. Mkandariwe pia alisisitiza ushirikiano kwa nchi wanachama katika kusimamia vyema michezo kwa nchi wanachama ili kundi kubwa la vijana lipate ajira kupitia sekta hiyo ambayo inatajwa kuwa njia mojawapo wa kuinua uchumi wa vijana.

Nchi nyingine ambayo ilikua inaomba uwenyeji wa mashindano hayo ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambayo baadae ilijitoa katika kinyang’anyiro hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!