Home Kitaifa MISIKITI IFUNDISHE VIJANA DINI NA KUTATUA CHANGAMOTO ZA JAMII.

MISIKITI IFUNDISHE VIJANA DINI NA KUTATUA CHANGAMOTO ZA JAMII.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema kazi za Misikiti ukiacha kufanya ibada ya sala pia wana jukumu la kutatua changamoto zinazoikabili jamii pamoja na kufundisha Dini kwa vijana.

Amesema Serikali ina wajibu wa kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Misikiti hiyo.

Rais Alhajj Dkt.Mwinyi amesema hayo alipoufungua Msikiti Sheikha Naema Bint Mohamed Al qasimi na kujumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe :29 Disemba 2023.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amewashukuru wafadhili familia ya Sheikha Naema Bint Mohamed Al qasimi kwa kujenga Msikiti na Madrasa zake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!