Home Kitaifa MIRADI YENYE THAMANI YA BILIONI 19.9 KUPITIWA NA MBIO ZA MWENGE WA...

MIRADI YENYE THAMANI YA BILIONI 19.9 KUPITIWA NA MBIO ZA MWENGE WA UHURU MOROGORO

Jumla ya miradi 70 yenye thamani ya shilingi bilioni 19.9 itapitiwa na mbio za mwenge ambapo miradi 18 itawekewa mawe ya msingi, 11 itafunguliwa,18 itazinduliwa na miradi 23 itakaguliwa na kuonwa.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima wakati wa mapokezi ya mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Matilda Buriani katika Kata ya Mziha iliyopo Wilaya ya Mvomero ambapo tayari utaanza mbio zake katika Mkoa wa Morogoro

Mwenge huo utakimbizwa Wilaya zote saba (7) za Mkoa huo zenye Halmashauri tisa (9) na kuhitimisha mbio hizo Mkoani Morogoro, Mwenge huo utakabidhiwa Mkoani Pwani aprili 29, mwaka huu ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro DC.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!