Home Kitaifa MIRADI YA MAJI 1029 KUTEKELEZWA VIJIJINI.

MIRADI YA MAJI 1029 KUTEKELEZWA VIJIJINI.

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amesema Serikali imepanga kutekeleza jumla ya miradi 1029 ya maji vijijini ambapo miradi 648 ni miradi inayoendelea kutekelezwa na miradi 381 ni mipya. Aidha, miradi 175 imepangwa kutekelezwa maeneo ya mijini.

Mheshimiwa Mahundi amesema hayo wakati akieleza vipaumbele vya sekta ya maji jijini Dodoma kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

Amesema wizara ina matumaini makubwa kufikia malengo kutokana na uongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ameonesha nia ya dhati ya kuhakikisha mama wa Kitanzania anatuliwa ndoo ya maji kichwani.

Kuhusu ubora wa maji yanayopelekwa kwa wananchi amesema kuwa Wizara kupitia maabara zake 17 za ubora wa maji nchini itaendelea kuhakiki na kufuatilia ubora wa maji katika vyanzo vya maji na mitandao ya kusambaza maji mijini na vijijini kwa lengo la kuhakikisha watumiaji wa maji wanapata huduma ya maji yanayokidhi ubora.

“Matumaini yetu ni kuhakikisha maagizo tuliyopewa kupitia Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi inafikiwa.” Mheshimiwa Mahundi amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!