MILIONEA MPYA MJINI : Lovenes Conrad Malias Mkazi wa Mbezi Jijini Dar Es Salaam akikabidhiwa mfano wa Hundi ya MILIONI TANO na Bwn. Robert Kasulwa Meneja wa Tigo Kanda ya Ubungo , Ikumbukwe Lovenes ni miongoni mwa WASHINDI wawili wa Milioni Tano Tano wiki ya nane Promosheni ya Cha Wote.
Na Mwandishi Wetu.
Lovenes Conrad Malias Mkazi wa Mbezi Kibanda Cha Mkaa Jijini Dar Es Salaam ni miongoni mwa washindi wa Milioni TANO Kampeni ya Tigo CHA WOTE wiki ya Nane ambapo hadi sasa Tigo wameshatoa Fedha Taslim na zawadi mbalimbali kwa Washindi zaidi ya elfu 17 Nchi Nzima tangu kampeni hii izinduliwe.
Akizungumza Leo Agosti 23 , 2023. Wakati wa Kumkabidhi Mshindi Loveness Mfano wa Hundi ya Milioni Tano maeneo ya Stendi Kimara Mwisho Jijini Dar Es Salaam , Meneja Wa Tigo Kanda ya Ubungo Bwn. Robert Kasulwa amesema kuwa hadi sasa ikiwa ni wiki Nane tu tangu Kampeni iyo izinduliwe wameshapatikana washindi zaidi ya elfu 17 kutoka maeneo mbalimbali nchini .
” Leo tunayo furaha kubwa kumkabidhi Loveness Milioni Tano yake , Lakini niwakumbushe Watanzania kwamba kila siku CHA WOTE inatoa zawadi ikiwemo pesa taslimu hadi Milioni Moja kwa washindi 320 kila siku , Pamoja Na zawadi za dakika na SMS kwa watumiaji wa Mtandao wa Tigo, kuibuka mshindi ni rahisi tu unachotakiwa ni kufanya miamala na Tigo Pesa kama Kutumia Lipa Kwa Simu , Kununua Vifurushi , Kulipia Bili kwa Tigo Pesa , n.k kwa kufanya ivyo nawewe siku si nyingi utakua miongoni mwa Washindi wa Kampeni hii ya CHA WOTE “. maana bado washindi zaidi ya elfu 10 wanatafutwa” amesema
Naye kwa Upande Wake Loveness mmoja wa washindi WA Milioni Tano , ameipongeza sana Kampuni ya Tigo kwa zawadi hii na kusema kuwa Milioni TANO hii itamsaidia kutimiza ndoto yake kubwa ambayo hakutaka kuiweka wazi
” Mimi ni mtumiaji wa TIGO wa muda mrefu na huwa na Tumia sana LIPA KWA SIMU ya TIGO labda huenda ndo maana nimeshinda milioni tano Leo, Kwakweli asanteni sana na nawasihi watanzania wafanye miamala kwa wingi, kununua vifurushi na Lipa kwa Simu maana ndo siri pekee ya Ushindi ” Alimalizia Loveness