Home Kitaifa MIKOA 26 KUSHIRIKI MASHINDANO YA KUHIFADHI NA KUSOMA QUR’AN

MIKOA 26 KUSHIRIKI MASHINDANO YA KUHIFADHI NA KUSOMA QUR’AN

Na. Magrethy Katengu

Watanzania wote bila kuangalia itikadi zao za kidini nchini Wameshauriwa kushiriki kwa wingi katika mashindano ya kuhifadhi Qur-an yanayotarajiwa kufanyika Machi 26 mwaka huu katika Ukumbi wa DYCC Temeke Jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mlezi wa Madrasa ya Tanzania Annujuum Islamic Center Maulid Kitenge ambapo amesema kuwa mashindano hayo yanaleta chachu Kwa watu kupenda kusoma vitabu vya dini kwa hiari yao wenyewe huku ikisaidia Jamii kuwa na maadili mema kwani wanaosoma vitabu vya dini inawasaidia kuwa na mwenendo mzuri.

Natambua umuhimu wa kusoma Qur- an Tukufu katika mwezi huu wa Ramadhan Mimi kwa kushirikiana na walezi wengine tumeamua kuweka mashindano ya kitaifa ya Qur -ani yatakayoshirikisha madrasa ya mikoa yote nchini Tanzania” amesema Kitenge

Hata hivyo amesema Mashindano hayo hayajawahi kutokea nchini Tanzania kwa sababu yanashirikisha Madrasa yote ya kiislamu lengo kubwa ni kuonesha umma umuhimu wa kusoma Qur -an na kutafuta utukufu na fadhila za Mwenyezi Mungu katika kipindi hiki cha Ramadhani

“Tayari tuna viongozi mbalimbali watakaoshiriki katika mashindano haya ikiwa ni pamoja Mheshimiwa Abdalla Ulega, Hawa Ghasia, Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Tanga Alshayma pamoja na kamanda Kanda maalum ya dar es salaam Jumanne Muliro”, amesema Kitenge.

Naye Mlezi wa Madrasa Irene Kilenga (baby mama) ameomba Wamama kutoka sehemu mbalimbali kushiriki katika mashindano ili kuweza kusikia nakuona vijana na watoto wadogo walivyoweza kuhifadhi na kusoma kitabu cha Qur-ani Tukufu.

Sisi kina mama ndio walezi wa watoto hawa hivyo ni vyema wote tukajitokeza kwa wingi kuona namna watoto walivyoweza kuhifadhi Qur-an na kuweza kusoma ,tunaona watoto wengi wameingia katika dimbwi la muziki lakini kupata watoto walokubali kuketi kusoma na kukariri Qur-ran Jambo jema ,”amesema Baby Mama.

Amesema huu ni wakati wa kutafuta faradhi za Allah kwa kuyatukuza maneno yake pamoja na kuacha makatazo yae

Aidha zawadi mbalimbali zitatolewa kwa Washiriki watakaoshinda Mashindano hayo lakini pia kutakuwepo na viongozi mbalimbali wa kiserikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!