Home Kitaifa MIKATABA MINNE YA UJENZI WA BARABARA YENYE THAMANI YA BILIONI 10.75 YASAINIWA...

MIKATABA MINNE YA UJENZI WA BARABARA YENYE THAMANI YA BILIONI 10.75 YASAINIWA DAR ES SALAAM

Na Magrethy Katengu – Dar es salaam

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imesaini mikataba minne ya miundombinu ya barabara yenye thamani ya bilioni 10.75 zitakazojengwa kwa kiwango cha lami ujenzi wake utaanza muda wowote kuanzia sasa na kukamilika ndani ya mwaka mmoja .

Ameyasema hayo leo Julai,15, 2024 Jijini Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto katika hafla ya utiaji saini mikataba hiyo ambapo amewaagiza wakandarasi waliongia mikataba kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na muda waliopewa ili kusitokee mkanganyiko baina ya serikali na wananchi kulalamikia ubovu wa miundombinu wakati fedha zimeshatolewa.

“Leo tumeshuhudia utiaji saini huu wa ujenzi wa miradi hii ya barabara hizi fedha zote zinatokana na kodi za wananchi hivyo nisingependa kuona ujenzi unachukua muda mrefu kukamilika alafu wakati mwingine kutumia muda kufuatiliana huku mmeomba wenyewe mkiwa mmejihakikishia mnaweza sitokubali hali hii ijitokeze nitakuwa mbogo kwenu miradi ikisuasua ” amesema Kumbilamoto

Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Jomaary Satura amebainisha miradi hiyo ya ujenzi wa wa barabara (0.39km) kiwango cha lami Sukita (0.5km) ,Mwanza (0.27km),Dodoma (0.28km) Udowe (0.48km) , Magengeni -Chang’ombe, Afrikan school -Sanene (0.5 km) jumla ya ujenzi wa barabara utagharimu kiasi cha zaid ya billion 3 na Mkandarasi wake ni Kampuni ya M/S SOUTHERN LINKS LIMITED

Zabuni ya ujenzi karavati /Msumi bombambili, Kavesu Liwiti kwa mzava na kisukulu ambapo ujenzi huo utagharimu zaidi billion moja na mkandarasi wake ni M/ S CROSS WOURLD CO LTD

Na Zabuni ya Barabara ya Pugu -Majohe -Mbondole-Viwege (0.4km) kwa kiwango cha zege na Barbara ya Kimanga -Mazda(0.4km) kwa kiwango cha lami ambapo utagharimu kiasi cha zaidi ya billion 1na Mkandarasi wake M/S OSAKA COMPANY (T) LIMITED

Ujenzi wa barabara ya Talian (0.5km), Masai wawili (0.3km), Soko la kigogo (0.15 km), Pugu kanisani Katoliki (0.1km) Pugu -Majohe- Mbondole (0.75km) kwa kiwango cha lami ujenzi utagharimu kiasi cha Zaidi ya billion 1, na Mkandarasi wake atakeyejenga M/S SOURTHERN LINKS LIMITED

Pia Ujenzi wa barabara ya kwa Mpalange -Mwanagati-,Kitunda(0.5km) kwa kiwango cha lami, Kiyombo Kipera (0.2km) kiwango cha zege ambapo ujenzi huo wote utagharimu zaidi ya billion 1 na Mkandarasi wake ni M/S SOURTHERN LINKS LIMITED

Sanjari na hayo Ujenzi wa barabara ya Moshi (0.27 km) kwa kiwango cha lami ambapo utagharimu zaidi ya milioni 4 Mkandarasi wake ni M/S AM& PARTNERS LIMITED

Na ukarabati wa barabara mbalimbali ndani ya halmashauri ” Maintenance and spot improvement of acces roads to the community facilities in Dar es salaam city council utagharimu zaidi ya milioni 4 na Mkandarasi wake ni M/S NYAKARUNGU CIVIL WORKS CONTRACTOR LIMITED

Pia Zabuni ya kujenga barabara ya TI.TANICI ( 0.222km) ,TAITANIC 2 ( 0.106) kwa kiwango lami itagharimu zaidi ya billion 4 M/S CROSSWORLD CONSTRUTION COMPANY LIMITED

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo amesema amesema mikataba hii imesainiwa mbele ya vyombo vya habari ni jambo la msingi kwani wanaotoa kodi zao wanaona zinapokwenda hivyo amewasihi wakandarasi wasiwaangushe wazingatie muda wa mikataba yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!