Home Kitaifa MIKAKATI KUENDELEZA NCHI MASIKINI ZAIDI KUSAIDIA UBORESHAJI WA SERA

MIKAKATI KUENDELEZA NCHI MASIKINI ZAIDI KUSAIDIA UBORESHAJI WA SERA

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema Mikakati Madhubuti wa Kuendeleza Sekta za Uzalishaji Nchi maskini zaidi Afrika itasaidia kuboresha Sera na Mikakati ya kuendeleza sekta za uzalishaji katika nchi hizo kusomana na kutekelezeka kwa ufanisi.

Kigahe ameyasema hayo Oktoba 12, 2022 wakati akifungua Warsha ya Kikanda ya Mkakati Madhubuti wa Kuendeleza Sekta za Uzalishaji katika nchi maskini zaidi Afrika uliofanyika jijini Dar es salaam.

Amesema Mikakati hii inayoandaliwa itasaidia katika uhuishaji wa Sera, Sheria na mikakati mbalimbali nchini ili kuiendeleza Sekta ya uzalishaji hususani katika kuongeza thamani mazao ya kilimo hususani mazao yanayozalisha sukari, mafuta ya kula, ngano na nguo.

Aidha, amewashauri watanzania kuzalisha bidhaa bora na zinazokidhi viwango vya kimataifa kwa wingi ili ziweze kuingia katika ushindani wa kibiashara kitaifa, kikanda na kimataifa hususani katika soko la Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA)

Naye Mkurugenzi wa Repoa Bw. Donald Mmari amesema REPOA imefanya utafiti katika maeneo ya uzalishaji wa mafuta ya kula, nguo na vifaa vya ujenzi ambapo mapendekezo ya utafiti huo yatachangia katika kuboresha utungaji na uhuishaji wa Sera zitakazoongeza tija katika sekta za uzalishaji.

Aidha, Bw. Mmari amesema warsha hiyo iliyohudhuriwa na washiriki kutoka Tanzania, Rwanda, Zambia, Zimbabwe, Botswana, Burkinafaso, Rwanda, Togo, Afrika ya Kusini, Mauritius na Singapore itaboresha mikakati hiyo madhubuti ili iweze kutatua changamoto mbalimbali na kuendeleza sekta za uzalishaji katika nchi maskini zaidi Afrika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!