Imeelezwa kuwa migogoro wa kiuongozi uliopo katika Chama cha wafugaji Tanzania unasababisha wafugaji nchini kushindwa kufuga kisasa jambo ambalo linapelekea sekta hiyo ya mifugo  kushindwa kuchangia  kwa kiwango kinachoridhisha katika pato la Taifa.
Hayo yameelezwa Aprili 27 na baadhi ya wafugaji mkoani Morogoro akiwemo Shambakubwa Longido wakati wakizungumza na vyombo vya habari juu ya taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi wa Chama cha wafugaji hapa Nchini ikieleza kufutwa kwa uchaguzi uliofanyika Aprili 8 mwaka 2024 ambapo wamesema mgogoro huo hauna tija kwa masilahi ya wafugaji hapa Nchini.
Wamesema kwa sasa wanachama wa chama cha wafugaji hapa Nchini wamekumbwa na taharuki juu ya kufutwa kwa uchaguzi huo ambapo wamesisitiza kuwa ili uchaguzi uweze kufutwa ni lazima taratibu zifatwe na wafugaji wote wajulishe.
Baada ya kufanya mawasilianao na waliokuwa wajumbe wa kamati huru ya uchaguzi wa Chama cha Wafugaji hapa Nchini ambao ni Ole Mkulago ambaye ni Katibu, Alhaji Marussu na Shambakubwa Longido kwa pamoja wamesema uchaguzi huo ulifanyika kwa kufuata taratibu, sheria na kanuni na hakukuwa na changamoto yeyote ambayo ingesababisha uchaguzi huo kufutwa.
Aidha wajumbe hao wamesema kitendo kilichofanywa na aliyekuwa mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi kufuta matokeo ya uchaguzi bila kushirikisha wajumbe wa tume ni kinyume na katiba pamoja na kanuni za uchaguzi za  chama cha wafugaji hapa Nchini.
Ikumbukwe hivi karibuni aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume huru ya uchachaguzi Charles Malagwa alitangaza kufuta matokeo ya Uchaguzi wa Chama cha Wafugaji Tanzania ambao ulifayika tarehe 8 Aprili 2024 ambao uliwaweka madarakani Murida Mshota kama mwenyekiti wa Chama, Kusundwa Wamalwa ambaye ni Makamu Mwenyekiti, na Mathayo Daniel ambaye alichaguliwa kuwa katibu Mkuu wa Chama cha Wafugaji Tanzania.